Aug 29, 2024 07:38 UTC
  • Shahrivar Nane; Siku ya kupambana na ugaidi nchini Iran

Leo, Alhamisi, tarehe 8 Shahrivar sawa na Agosti 29, 2024 ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi Rais na Waziri mkuu wa Iran, na ni siku ya kitaifa ya kupambana na ugaidi nchini Iran.

Tarehe 8 mwezi Shahrivar mwaka1360 Hijria shamsia kwa mujibu wa kalenda ya Iran inayosadifiana na tarehe 30 Agosti mwaka 1981 ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi  Rais Mohammad Ali Rajaee na Mohammad Javad Bahonar Waziri Mkuu wa wakati huo wa Iran  pamoja na wawakilishi wengine wa serikali katika mlipuko uliotokea katika ofisi ya Waziri Mkuu. 

Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1997, zaidi ya raia elfu 17 na maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliuawa shahidi na kundi la kigaidi la Munafiqin na vijikundi vingine vya ugaidi. 

Baada ya kuanzisha hujuma za kigaidi nchini Iran, wanachama wa kundi hilo la kigaidi kwanza walikimbilia Paris na kisha Iraq.  

Mwaka 1991 na 1992, Saddam, dikteta wa zamani wa Iraqi, aliwatumia mamluki wa Munafiqin kuwakandamiza Wakurdi na kupanga mauaji ya kimbari ya raia hao wa Iraq ambapo maelfu kadhaa ya wanawake na watoto waliuawa kwa umati. 

Dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein

Licha ya vitendo vyote vya uharibifu vinavyofanywa na baadhi ya nchi za Magharibi, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni taifa lisilopingika katika kukabiliana na ugaidi duniani. Iran hivi sasa mbali na kuwaunga mkono majirani zake katika vita dhidi ya ugaidi inashirikiana pia kwa uaminifu na kwa busara na taasisi na mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi katika mapambano dhidi ya ugaidi. 

 

Tags