Iran yaboresha mfumo wa hali ya juu wa ulinzi
Kamanda wa ngazi za juu katika Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIADF), ambacho ni tawi la Jeshi la Iran, ametangaza kuimarishwa mojawapo ya mifumo ya juu zaidi ya ulinzi katika kikosi hicho.
Brigedia Jenerali Mohammad Yousefi Khoshqalb, naibu kamanda anayesimamia uratibu katika Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Iran, ametangaza Jumatatu kwamba kumetekelezwa hatua za kuimarisha na kuboresha mfumo wa ulinzi wa anga uliopewa jina la Rasoul.
Mfumo huo ulioundwa kikamilifu nchini ulijiunga na mtandao jumuishi wa ulinzi wa anga wa Iran Desemba mwaka jana baada ya kufanyiwa majaribio. Mfumo huo unajumuisha ndege ndege zisizo na rubani hasa aina ya Karrar na nyingine ya masafa marefu yenye kusheheni makombora aina ya Majid ya anga kwa anga.
Akizungumzia uboreshaji uliotekelezwa katika mfumo huo tangu kuzinduliwa kwake, kamanda huyo alidokeza uboreshaji wa aina mbalimbali za uendeshaji wa ndege hiyo isiyo na rubani, ikiwa ni pamoja na uwezo mkubwa zaidi wa mfumo wa rada wa ndege hiyo.
Kwa mujibu wa Khoshqalb, ndege hiyo pia sasa inaweza kuwa na makombora mengi tofauti tofauti mbali na Majid ambayo yanaweza kutumwa kwa mujibu wa hali ya eneo la vita.
Pia siku ya Jumatatu, Kamanda wa ngazi za juu katika Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Alireza Sabahifard, alisema mifumo hiyo ya ulinzi imeundwa pamoja na kuwepo na vikwazo vya miongo kadhaa viliyowekwa na nchi na Magharibi.