Iran kufuta tuzo ya FIFA kwa Trump?
-
Trump kupokonywa tuzo ya amani ya FIFA?
Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, baada ya kusababisha hasara za kiuchumi na kutia doa hadhi ya kijeshi na kisiasa ya Marekani sasa vimeweka kivuli kizito juu ya kinachoitwa tuzo ya amani ya FIFA kwa rais Donald Trump.
Kwa mujibu wa mwandishi wa michezo wa Shirika la Habari la Fars, tuzo ya amani ya FIFA ambayo rais wa Shirikisho hilo la Mpira wa Miguu, Gianni Infantino, aliikabidhi kwa Trump bila uwazi na bila vigezo maalumu, sasa iko katika hatari ya kufutwa kutokana na sera zake za kivita. Ripoti iliyochapishwa Jumanne na gazeti la The Athletic imasema, malalamiko rasmi ya rais wa Shirikisho la Soka la Norway yamezindua mchakato wa kufutwa tuzo hiyo.
Baada ya kupokea tuzo hiyo ya kinachoitwa amani, Trump alishambulia nchi mbili—Venezuela na Iran—jambo ambalo limezua maswali mengi juu ya uhalali wa FIFA katika kutoa tuzo hiyo.
Kabla ya hapo, wanachama wengi kati ya 212 wa FIFA walikuwa wamepinga utoaji wa tuzo hiyo ya kubuniwa eti ya amani ambayo Infantino alimkabidhi rafiki yake wa karibu, Donald Trump.
Wataalamu wengi wa soka wanaamini kuwa tuzo hiyo haina hadhi yoyote kwa sababu haina vigezo vya wazi vya kumpata mshindi, na imekuwa ikitolewa kwa upendeleo na matakwa ya rais wa FIFA.
Aidha, mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran kwa ushirikiano na Israel yamepelekea kutiliwa shaka asili na hatua ya kutolewa tuzo hiyo kabla ya mashindano ya Kombe la Dunia, na mashabiki wengi wa soka wanaamini Marekani inayochochea vita haistahili kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia.
Sasa Lise Klaveness, rais wa Shirikisho la Soka la Norway, anasema anataka tuzo ya amani iliyotolewa na FIFA kwa Trump ifutwe, na tayari ameandaa malalamiko ya kimaadili dhidi ya Infantino, rais wa FIFA.
Kwa mujibu wa ripoti ya The Athletic, mpango huu unatarajiwa kuwasilishwa na rais wa Shirikisho la Soka la Norway katika kikao cha Kongamano la FIFA Alhamisi ijayo ili ujadiliwe.