Kan'ani: Chokochoko za adui dhidi ya Iran 'hazitapita bila jibu'
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i117044-kan'ani_chokochoko_za_adui_dhidi_ya_iran_'hazitapita_bila_jibu'
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran aliyemaliza muda wake ameonya kwamba vitendo vyovyote vya chokochoko dhidi ya mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu na umoja wa ardhi yake havitapita bila kujibiwa.
(last modified 2024-10-03T00:53:05+00:00 )
Oct 03, 2024 00:53 UTC
  • Kan'ani: Chokochoko za adui dhidi ya Iran 'hazitapita bila jibu'

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran aliyemaliza muda wake ameonya kwamba vitendo vyovyote vya chokochoko dhidi ya mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu na umoja wa ardhi yake havitapita bila kujibiwa.

Nasser Kana'ani ametoa kauli hiyo katika akaunti yake ya X ya mtandao wa kijamii siku ya Jumatano, baada ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kumimina makombora katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel ili kulipiza kisasi mauaji ya hivi karibuni ya utawala huo ghasibu dhidi ya viongozi wakuu wa muqawama au mapambano ya Kiislamu.

 Iran imechukua hatua imara kwa kuzingatia Kifungu cha 51 cha Hati ya Umoja wa Mataifa, kinachoelezea haki halali ya kila nchi kujilinda dhidi ya wavamizi wakaidi."

Msemaji huyo amepongeza "ushujaa, uwezo na mamlaka ya kiulinzi" ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vile vile msimamo na ukamanda thabiti wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei kuwa ni "chimbuko la fahari na utu" kwa Wairani wote.

Kanani amesisitiza kuwa Iran imejitolea kwa ajili ya utulivu na usalama wa eneo hili na itachukua hatua kali dhidi ya wavamizi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amebaini kuwa: "Utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake wanapaswa kujua kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatekeleza kivitendo inayoyasema. Hakuna hatua zozote za kichokozi dhidi ya mamlaka ya kujitawala  na usalama wa taifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zitapia bila kujibiwa."

Amesisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu kwa mara nyingine tena imethibitisha kwamba inaweza kufikia eneo lolote inalotaka na kuongeza kauwa: “Matarajio ya mustakabali wa eneo hili na Asia ya Magharibi yataamuliwa na wamiliki wa eneo hili na mataifa yake ya kihistoria na yenye mizizi, na sio wasio na mizizi, wavamizi na maghasibu."