Waziri wa Ulinzi wa Iran akutana na mwenzake wa Syria
Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Azizi Nasirzadeh, ambaye yuko ziarani nchini Syria, amekutana na na kufanya mazungumzo na waziri mwenzake leo Jumapili.
Waziri wa Uulinzi wa Iran anazuru Damascus kwa mwaliko wa mwenzake, Ali Mahmoud Abbas.
Brigedia Jenerali Azizi Nasirzadeh, anatazamiwa kukutana na maafisa wakuu wa Syria kwa mazungumzo ya kuimarisha uhusiano wa kiulinzi na kiusalama baina ya pande mbili za ushirikiano kati ya Iran na Syria.
Amesema "Syria ina jukumu la kimkakati katika sera ya kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran" na kuongeza kuwa: “Lengo letu ni kuainisha mikakati ya kuimarisha sekta hizi. Natumai, uhusiano kati ya nchi hizo mbili utabadilika kwa njia ambayo tunaweza kutoa msaada wa pande zote katika hali nyeti."
Katika ziara yake ya siku mbili, Waziri wa Ulinzi wa Iran anatazamiwa kukutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad na maafisa wengine wa kijeshi na kisiasa.
Ziara ya Nasirzadeh nchini Syria inafanyyika siku chache baada ya Ali Larijani, mshauri mkuu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, kutembelea Damascus na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Syria, akiwemo Rais Assad na Spika wa Bunge la Wananchi wa Syria, Hammoudeh Sabbagh.