Iran: Muqawama nchini Lebanon si kitu kinachoweza kufutwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121324-iran_muqawama_nchini_lebanon_si_kitu_kinachoweza_kufutwa
Balozi wa Iran nchini Lebanon amesema kuwa, Wawakilishi wa Hizbullah na harakati ya Amal walifanya mazungumzo na Joseph Aoun katika ule muda wa baina ya vikao viwili vya upigaji kura katika bunge na kupewa dhamana ya kutoguswa masuala hayo. Kwa kuzingatia hayo tunasema kwa kinywa kipana kwamba Muqawama hauwezi kamwe kufutwa nchini Lebanon.
(last modified 2025-01-11T23:33:22+00:00 )
Jan 11, 2025 23:33 UTC
  • Iran: Muqawama nchini Lebanon si kitu kinachoweza kufutwa

Balozi wa Iran nchini Lebanon amesema kuwa, Wawakilishi wa Hizbullah na harakati ya Amal walifanya mazungumzo na Joseph Aoun katika ule muda wa baina ya vikao viwili vya upigaji kura katika bunge na kupewa dhamana ya kutoguswa masuala hayo. Kwa kuzingatia hayo tunasema kwa kinywa kipana kwamba Muqawama hauwezi kamwe kufutwa nchini Lebanon.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Balozi Mojtaba Amani akibainisha hayo na kusema: “Kinachoenezwa katika propaganda kwamba Muqawama umetoweka si kweli. Muqawama una nguvu kwa sababu kama si uungaji mkono wa wawakilishi wa Muqawama, rais (wa Lebanon) asingechaguliwa na hili ni suala muhimu sana." 

Balozi wa Iran nchini Lebanon amesema hayo katika mahojiano maalumu ya moja kwa moja na Kanali la Habari ya Televisheni ya IRIB na kusisitiza kwamba: "Nchini Lebanon, rais na maafisa wengine lazima wawe na uhusiano mzuri na makundi tofauti."

Balozi Mojtaba Amani

 

Balozi Amani vile vile amezungumzia uhusiano uliopo kati ya rais mpya wa Lebanon na Hizbullah na kusisita kwamba, wakati Joseph Aoun alipokuwa kamanda wa jeshi la Lebanon, aliiheshimu sana Hizbollah na Muqawama. 

Ametoa mfano wa kuthibitisha uhakika huo akisema: "Katika tukio linalojulikana kwa jina la Kahaleh, Joseph Aoun alisimamia silaha kufika kwa Hizbullah baada ya kupinduka lori la Muqawama lililokuwa limepakia silaha hizo. Ushirikiano huo wa jeshi la Lebanon na Hizbullah ulipongezwa sana na ulikuwa na taathira kubwa hasa katika kuimarisha uhusiano mzuri baina ya pande hizo mbili" 

Akielezea muundo wa kikabila nchini Lebanon, Balozi Amani amesema: Kwa mujibu wa makubaliano ya kikaumu na kikabila, rais wa Lebanon lazima awe Mkristo wa Kimaroni, Waziri Mkuu awe Msuni na Spika wa Bunge awe Mshia. Yaani haiwezekani kundi lisilohusika na kuwa na kiongozi wa sehemu fulani, kuteua mtu wa kushika nafasi hiyo. Hali hiyo inalazimisha kila kiongozi kuwa na uhusiano mzuri na makundi yote.