Meja Jenerali Mousavi: Maneva yanayoendelea yanaonyesha utayarifu wa jeshi la Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121390-meja_jenerali_mousavi_maneva_yanayoendelea_yanaonyesha_utayarifu_wa_jeshi_la_iran
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran amesema kuwa, maneva ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na jeshi la Iran yadhihirisha kuwa tayari vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2025-01-13T08:10:21+00:00 )
Jan 13, 2025 08:10 UTC
  • Meja Jenerali Mousavi: Maneva yanayoendelea yanaonyesha utayarifu wa jeshi la Iran

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran amesema kuwa, maneva ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na jeshi la Iran yadhihirisha kuwa tayari vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu.

Meja Jenerali Sayyid Abdulrahim Mousavi Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran  amesema katika hafla ya kuziunganisha ndege zisizo na rubani 1,000 katika taasisi ya kivita ya jeshi la Iran kwamba: Kuongezwa ndege zisizo na rubani (droni) ni sehemu ya uwezo wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Kamanda Mousavi ameongeza kuwa: Uunganishaji huo, uzinduzi na maneva yanayoendelea kutekelezwa katika maeneo ya jiografia na bahari ya Iran yanaonyesha uwezo na utayari wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  

Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran amesisitiza kuwa ni vyema maadui wa Iran ya Kiislamu wasichezee kamari fursa yao na kueleza kuwa: Hapa kuna Iran ya Kiislamu inayojifakharisha; taifa kubwa la Iran halitashindwa kuhami malengo ya mapinduzi na heshima ya taifa. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa maneva ya pamoja ya  ulinzi wa anga ya 1403 ya jeshi la Iran chini ya kauli mbiu "Ya Ali Ibn Abi Talib (AS)" yalianza jana asubuhi yakiongozwa na kamandi ya Mtandao wa Pamoja wa Ulinzi wa Anga katika maeneo ya ulinzi wa anga ya magharibi na kaskazini mwa Iran huko Fordo na Khandab.