Araqchi: Asili ya makubaliano ya Iran na Russia ni ya kiuchumi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121598-araqchi_asili_ya_makubaliano_ya_iran_na_russia_ni_ya_kiuchumi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano ya kina ya kimkakati ya ushirikiano kati ya Iran na Russia yanahusu vipengee vyote vya uhusiano wa nchi na kwamba asili ya makubaliano hayo zaidi ni katika uga wa uchumi.
(last modified 2025-01-18T11:07:00+00:00 )
Jan 18, 2025 11:07 UTC
  • Sayyid Abbas Araqchi
    Sayyid Abbas Araqchi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano ya kina ya kimkakati ya ushirikiano kati ya Iran na Russia yanahusu vipengee vyote vya uhusiano wa nchi na kwamba asili ya makubaliano hayo zaidi ni katika uga wa uchumi.

Sayyid Abbas Araqchi amesema kuhusu makubaliano ya kina ya ushirikiano wa kimkakati kati ya Iran na Russia yaliyosainiwa jana katika ziara ya Rais Masoud Pezeshkian wa Iran nchini Russia kwamba: "Tuna matarajio makubwa kuwa kwa kutiwa saini makubaliano haya kuanzia sasa na kuendelea tutapiga hatua kwa urahisi katika nyanja za uhusiano wa kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni n.k na katika fremu moja na mazingira bora kwa ajili ya ushirikiano wa pande mbili. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema dhati ya makubaliano haya ni ya kiuchumi na kwamba yanajumuisha nyanja zote za kiuchumi, pamoja na biashara ya utalii, usafirishaji, n.k.

Mrais Pezeshkian na Putin

Araqchi ameongeza kuwa: Makubaliano haya pia yamejumuisha nyanja za utamaduni, sayansi, sheria, mawasiliano na n.k. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa, katika ziara yake nchini Russia, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametia saini makubaliano ya kina ya ushirikiano wa pamoja wa kimkakati ya kati ya nchi mbili.