Kiongozi Muadhamu: Ni muhimu kutoa taswira ya sifa na mienendo ya mashahidi
(last modified Fri, 24 Jan 2025 04:12:16 GMT )
Jan 24, 2025 04:12 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Ni muhimu kutoa taswira ya sifa na mienendo ya mashahidi

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kuna umuhimu wa kuonyesha sifa na tabia za mashahidi katika kazi za kitamaduni na sanaa.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema hayo katika kikao na waandaaji wa Kongamano la Kitaifa la kumbukumbu ya mashahidi 1880 wa Kashan kilichofanyika Januari 15, na habari yake kutangazwa usiku wa jana katika ukumbi wa mkutano huo huko Kashan.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutaja kudhihirisha tabia za mashahidi katika kazi za kiutamaduni na kisanaa kuwa ni jambo la dharura na akaongeza kuwa: Sifa maalumu, suluki, mienendo na sifa bora za kitabia kama vile kujitolea mhanga kwa mashahidi, ibada na kunyenyekea vijana wapiganaji kwa Mwenyezi Mungu na heshima  na ghera yao kwa kaulimbiu za Uislamu na mapinduzi ni hitajio la kudumu la taifa ambapo uhamishaji wa tabia hizi unawezekana kupitia kazi na athari za kisanii na uzalishaji wa kazi zenye ubora kama vile filamu, mashairi na picha za kuchora.

Kuonyesha subira na shukurani za mama wa mashahidi lilikuwa suala jengine ambalo kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza juu ya kuyasawiri kwa njia za kisanii akisema: Subira na shukurani za mama aliyemtoa mtoto wake au watoto wake katika njia ya Mwenyezi Mungu haziwezi kuelezewa kama inavyotakiwa, lakini kuonyesha masomo haya ya kushangaza kunawezekana kupitia kazi za sanaa.

Kiongozi Muadhamu akiwa katika kikao na waandaaji wa Kongamano la Kitaifa la kumbukumbu ya mashahidi 1880 wa Kashan

 

Ayatullah Khamenei pia amesema, mji wa Kashan ulioko katika mkoa wa Isfahan, katikati mwa Iran, katika historia yote umekuwa ukilea na kutoa wanazuoni, mafakihi, wapiganaji na wasanii.

Sambamba sambamba na kuthamini na kuenzi kumbukumbu za shakhsia waliopigana dhidi ya wakoloni wa Uingereza walioibuka kutoka mji huo hasa Marehemu Ayatullah Kashani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: mji wa Kashan mbali na kuwa mashuhuri katika sayansi, sanaa na kushikamana na Ahlul-Bayt (AS), pia iling'ara katika kipindi cha Kujihami Kutakatifu na baadhi ya matukio mengine ya mapinduzi na kuonesha kwamba uleaji na uandaaji wa watu wanamapambano na watu jasiri unaendelea katika eneo hilo.