Imam Khamenei: Ushindi wa wananchi wa Gaza ulikuwa ushindi dhidi ya Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, ushindi wa wananchi wa Gaza ulikuwa ushindi dhidi ya Marekani.
Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema hayo leo alipokutana na Mkuu na wajumbe wa Baraza la Uongozi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS).
Mwanzoni mwa mkutano huo, Mohammad Ismail Darwish, Mkuu wa Baraza la Uongozi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS alitoa pongezi kwa ushindi mkubwa wa muqawama wa Gaza na kumhutubu kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa kumwambia: Tunachukulia kusaidifiana siku za ushindi wa muqawama wa Ghaza na kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni dalili njema na tunatumai kwamba, kusadifiana huku kutakuwa msingi wa kukombolewa Quds na Msikiti wa Al-Aqsa.
Mwanzoni mwa kikao hicho pia, Khalil al-Hayya, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas sambamba na kutoa pongezi kwa Kiongozi Muadhamu kwa ushindi wa muqawama wa Gaza alisema: "Leo tumekuja kukutana nawe mhesghimiwa huku sote tukiwa tunajivunia, na ushindi huu mkubwa ni ushindi wa pamoja sisi na Jamhuri ya Kiislamu.
Katika kikao hicho Imam Khamenei sanjari na kuenzi kumbukumbu ya umbukumbu za mashahidi wa Gaza na makamanda waliouawa shahidi hususan shahidi Ismail Haniya amesema: Mwenyezi Mungu akupeni nyinyi na watu wa Gaza izza, heshima na ushindi, na aifanye Gaza kuwa mfano wa Aya tukufu ya Qur'ani isemayo: "Inawezekana kwa kundi dogo kushinda kundi kubwa na lenye nguvu kutokana na kufaulu na idhini ya Mwenyezi Mungu."Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Imam Khamenei amesisitiza zaidi kwa kusema: Nyinyi mliushinda utawala wa Kizayuni na kimsingi mliishinda Marekani na kwa neema ya Mwenyezi Mungu hamkuwaruhusu kufikia malengo yao yoyote.
Akizungumzia mateso ambayo watu wa Gaza waliyapata katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu wa muqawama, Imam Khamenei ameongeza kuwa: Matokeo ya mateso na gharama zote hizo hatimaye ni ushindi wa haki dhidi ya batili, na watu wa Ghaza wakawa ni mfano kwa wale wote ambao nyoyo zao zimejitolea kkwa ajili ya muqawama.