Iran yaanza kutoa kadi za benki kwa wageni kutoka nje
Benki za Iran zimeruhusiwa kutoa kadi za benki kwa wageni wanaotembelea nchi huku kukiwa na juhudi za kuimarisha utalii.
Ripoti ya shirika la habari la Tasnim imesema Benki Kuu ya Iran (CBI) imeziarifu benki za serikali na za watu binafsi nchini kwamba zinaweza kuanza kutoa kadi za benki kwa watalii na wageni wasio wakazi ili kuwaruhusu kulipia huduma na bidhaa kwa sarafu ya Iran.
"Raia wa kigeni wanaweza kubadilisha sarafu zao kwa rial kwa bei zilizoidhinishwa na mfumo wa CBI na kuweka fedha zao wenye akaunti iliyounganishwa na kadi ya malipo", CBI imesema katika agizo lake, na kuongeza kuwa salio katika kadi litabadilishwa na kurejeshwa kwa mgeni tarehe ya kumalizika muda wa kadi zao.
Kabla ya hatua hiyo kutangazwa, raia wa kigeni walilazimika kubeba kiasi kikubwa cha fedha wakati wa kuwepo kwao nchini Iran. Pia walilazimika kuuza sarafu zao kwa bei ya chini ili waweze kupokea pesa taslimu.
Benki Kuu ya Iran (CBI) iliidhinisha hatua hiyo mnamo Novemba mwaka jana.