Makampuni yanayotegemea elimu Iran yanavunja rekodi ya mapato
(last modified Tue, 06 May 2025 10:59:53 GMT )
May 06, 2025 10:59 UTC
  • Makampuni yanayotegemea elimu Iran yanavunja rekodi ya mapato

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Tathmini ya Makampuni yanayoendeshwa kwa kutegemea Msingi wa Elimu na Maarifa ya Iran ametilia mkazo nafasi muhimu ya makampuni hayo katika maendeleo ya teknolojia na viwanda humu nchini na kusema kuwa yamevunja rekodi ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi mwaka 2024.

Amir Younesian, amegusia jukumu kuu la makampuni yanayotegemea elimu na maarifa kuwa ndiyo nguvu inayosukuma mbele maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini Iran na kutangaza kuwa, katika kipindi cha mauzo cha mwaka 2024, makampuni hayo ya Iran yamevunja reko kwa kuuza nje bidhaa zenye thamani ya dola milioni 500 licha ya uchanga wa makampuni hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Tathmini ya Makampuni yanayotegemea Elimu na Maarifa ambayo iko chini ya Ofisi ya ya Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya Kisayansi, pia amesisitizia ulazima wa kuwekewa makampuni hayo miundombinu imara kwa ajili ya maendeleo ya sayansi na teknolojia humu nchini kwa kutegemea uzalishaji wa bidhaa za elimu na maarifa.

Kwa upande wake, mtafiti wa sera za viwanda nchini Iran, Barzin Jafartash Amiri amekosoa fikra za baadhi ya watu kuhusu sera ya viwanda nchini na kusisitizia jukumu kubwa la serikali katika sekta hiyo akitaka kufanyike mabadiliko sheria na sera za uchumi kwa manufaa ya wahusika wa masuala ya uchumi humu nchini.

Amesema, moja ya changamoto kubwa zinazopaswa kubadilishwa ni kuondokana kikamilifu na mauzo ya nje ya malighafi na badala yake mauzo yawe tu ya bidhaa za viwanda vya ndani ya Iran.