Umuhimu wa safari ya Araghchi nchini Pakistan
Seyyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana alifanya safari mjini Islamabad na kukutana na kushauriana na viongozi wa Pakistan kuhusu kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya kieneo na kimataifa.
Kwa kuzingatia hali ya hivi sasa ya India na Pakistan utayari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kusaidia kupunguza hali ya wasiwasi, safari ya hivi sasa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini Pakistan, jirani yake wa mashariki ina umuhimu wa kipekee.
Hii ni ziara ya pili ya Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya awamu ya 14 nchini Pakistani kwa. Mwaka jana 2024, Araqchi alifanya safari pia mjini Islamabad na kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa Pakistan.
Katika ziara yake ya siku moja mjini Islamabad, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alikutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati na tofauti na Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari na Waziri Mkuu Shahbaz Sharif kama ambavyo alifanya mazungumzo pia na Sayyid Asim Munir, Mkuu wa majeshi ya nchi hiyo.
Araqchi alipowasili mjini Islamabad alisema kuhusu malengo ya safari yake nchini Pakistan: "Uhusiano kati ya nchi hizo mbili una umuhimu mkubwa, kama ilivyo uhusiano wa Iran na nchi nyingine za eneo."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: "Hali ya eneo ni muhimu sana kwa Iran, na huku akitilia mkazo kupunguzwa mivutano ambapo alisema: Tunatoa wito kwa pande zote kujizuia na kuzuia hali kuwa mbaya zaidi." Araqchi alielezea matumaini kuwa ushirikiano kati ya Iran na Pakistan utachukua njia bora zaidi.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistani pia ilitangaza katika taarifa yake: Iran na Pakistan zinafurahia uhusiano wa karibu wa pande mbili uliokita katika historia ya pamoja, utamaduni na dini.

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran imelenga kuimarisha zaidi uhusiano uliopo na kuongeza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Taarifa hiyo iliendelea kusema: "Ziara hii ya ngazi ya juu inaakisi uhusiano wa kina na imara kati ya Pakistan na taifa ndugu na rafiki la Iran."
Reza Amiri Moghadam, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Pakistan ameashiria umuhimu wa kuendelea mashauriano na vikao baina ya maafisa wa nchi hizo mbili na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya kieneo na kimataifa na kusema: "Ziara ya Araqchi kwa jirani wa mashariki wa Iran ni hatua muhimu katika kuchora ramani ya njia ya kuendeleza ushirikiano kati ya Tehran na Islamabad."
Mohammad Mudassir Tipu," balozi wa Pakistan mjini Tehran pia alisema kuhusu umuhimu wa ziara ya Araqchi mjini Islamabad: "Tunaichukulia ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini Islamabad kuwa muhimu sana katika kipindi hiki kigumu, na tunathamini juhudi za jirani yetu muhimu Iran, katika kuimarisha maingiliano na maelewano kati ya nchi hizi mbili."
Akiashiria mashauriano ya hivi karibuni kati ya wakuu wa nchi za Iran na Pakistan, pamoja na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili kufuatia mvutano kati ya Islamabad na New Delhi, balozi wa Pakistan mjini Tehran ameongeza kuwa: Huku ikijizuia, Pakistan imetangaza kuwa iko tayari kufanya uchunguzi wa wazi na usiopendelea upande wowote kuhusu shambulio la hivi karibuni nchini India.
Uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan umekuwa ukiongezeka katika ngazi za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika miaka ya hivi karibuni. Mazingira ya kiutamaduni na kihistoria, na uhusiano mkubwa wa kisiasa kati ya Tehran na Islamabad, umesababisha kuongezeka mazungumzo ya pande mbili kati ya maafisa wa ngazi za juu wa nchi hizo mbili.
Pakistan imetoa njia mawasiliano ya China na Asia Kusini kupitia miradi inayohusiana na Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC), na kwa upande mwingine, ni mshirika wa kimkakati wa China, na hii itakuwa na ufanisi kwa Iran katika ushirikiano wa kikanda na China.

Iran na Pakistan ni nchi mbili za Kiislamu na wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na jumuiya kama vile ECO, ambayo imefungua njia ya maingiliano makubwa kati ya nchi hizo mbili.
Kwa kuzingatia kuwa Pakistan ni nchi yenye watu wengi na nchi hiyo inahitaji bidhaa za Iran hususan katika nyanja za kilimo, viwanda vya chakula na vifaa vya ujenzi, mikoa ya mpakani ya Iran inaweza kuwa lango la kuongeza mauzo ya nje na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na nchi hii.
Ziara ya Araqchi mjini Islamabad inafanyika wakati ambapo mvutano kati ya India na Pakistan umeongezeka kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi huko Kashmir inayodhibitiwa na India, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa kuzingatia uhusiano wake wa hali ya juu wa kisiasa na New Delhi na Islamabad, inaweza kutumia uwezo wake wa kidiplomasia kufanya upatanishi.
Kupanuliwa uhusiano kati ya Iran na Pakistan kutakuwa na nafasi ifaayo katika kujenga usalama na utulivu katika bara Hindi, na nchi hizo mbili zina misingi mwafaka ya kuendeleza uhusiano katika sekta mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.