Wayemen wasambaratisha sekta ya utalii ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i126046-wayemen_wasambaratisha_sekta_ya_utalii_ya_israel
Athari za tangazo la Jeshi la Yemen la kufunga anga ya Israel mpaka utawala wa Kizayuni utakapoacha kufanya jinai dhidi ya wananchi wa Ghaza zinaendelea kuitia hasara Israel na zimesambaratisha sekta ya utalii ya utawala wa Kizayuni.
(last modified 2025-05-06T02:45:35+00:00 )
May 06, 2025 02:45 UTC
  • Wayemen wasambaratisha sekta ya utalii ya Israel

Athari za tangazo la Jeshi la Yemen la kufunga anga ya Israel mpaka utawala wa Kizayuni utakapoacha kufanya jinai dhidi ya wananchi wa Ghaza zinaendelea kuitia hasara Israel na zimesambaratisha sekta ya utalii ya utawala wa Kizayuni.

Miongoni mwa hasara unazopata utawala wa Kizayuni ni kukwama ujenzi wa makumi ya maelfu ya nyumba za walowezi wa Kizayuni kwenye ardhi wanazoporwa Wapalestina. Sehemu kubwa ya bajeti ya nyumba hizo inatokana na sekta ya utalii.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la FARS unaonesha kuwa, kombora la Wayemen lililopiga karibu na Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion huko Tel Aviv limechimbua shimo kubwa lenye kina cha mita 25. Shirika hilo limeuliza swali kwa kuandika: "Hali ingelikuwaje kama kombora hilo lingesogea mita chache tu na kupiga karibu na ndege?"

Tayari mashirika mbalimbali ya ndege yamesimamisha safari zao za kuelekea Israel. Hadi wakati tunatayarisha taarifa hii, zaidi ya mashirika 20 ya ndege yalikuwa yamesimamisha safari zao kuelekea Israel suala ambalo limeitia hasara ya dola milioni 4 sekta ya utalii ya utawala wa Kizayuni. Netanyahu alikuwa ameanzisha mpango wa dola milioni 4 wa kufufua sekta hiyo iliyosambaratika kutokana na vita.

Mwaka jana 2024, Iran ilifanya mashambulizi mawili makubwa ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel yaliyopewa jina la Ahadi ya Kweli 1 na Ahadi ya Kweli 2. Mashambulizi hayo ya Iran yalipelekea mashirika ya nje kusimamisha safari zao kuelekea Israel. Sekta ya utalii ya utawala wa Kizayuni ilisambaratika kwa asilimia 80. Uchumi wa utawala wa Kizayuni uliingia hasara ya moja kwa moja ya mamilioni ya dola.