Ndege za Iran zimeimarishwa kwa makombora tuli ya masafa marefu
(last modified Fri, 09 May 2025 03:08:24 GMT )
May 09, 2025 03:08 UTC
  • Ndege za Iran zimeimarishwa kwa makombora tuli ya masafa marefu

Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Ndege zote za kivita za Jeshi la Anga zina silaha, vifaa na makombora ya kisasa ya masafa marefu yaliyotengenezwa humu humu nchini."

Akizungumza na waandishi wa habari jana Alkhamisi pambizoni mwa hafla ya kuwaenzi na kuwatambulisha makamanda wakongwe na wapya huko Dezful, Brigedia Jenerali Vahid Vahedi amesisitiza kuwa: Jeshi lenye nguvu la Anga la Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran liko katika kiwango chake cha juu uimara na liko tayari kutekeleza amri za Amirijeshi Mkuu wakati wowote ule.

Amesema: "Leo Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limejiandaa zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika masuala ya ukarabati, matengenezo na ufufuaji wa zana za kijeshi sambamba na kutoa mafunzo, nguvu kazi na kuzalisha zana za kisasa za hali ya juu."

Kamanda Vahedi amesema: "Kwa jitihada nzuri za sekta ya ulinzi ya nchi, leo hii Jeshi la Anga la Iran lina vifaa bora sana na aina mbalimbali za silaha za kisasa kabisa."

Amesisitiza kuwa majeshi ya Iran likiwemo Jeshi la Anga yataendelea kuilinda vilivyo nchi ikiwemo anga ya mfumo mtakatifu wa Jamhuri ya Kiislamu na Iran kwa mapenzi makubwa hadi tone la mwisho la damu.

Ikumbukwe kuwa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwemo Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel wanatoa vitisho vya mara kwa mara dhidi ya taifa hili la Kiislamu. Likini Iran iko imara kukabiliana na vitisho vyote hivyo.