Aug 07, 2016 13:59 UTC
  • Tehran na Baku zasaini hati sita za ushirikiano

Hati sita za makubaliano ya ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Azerbaijan zimesainiwa Jumapili hii huko Baku mji mkuu wa Azerbaijan ikiwa ni katika fremu ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi mbili.

Makubaliano ya ushirikiano kati ya Shirika la Taifa la Viwango la Iran na Wizara ya Uchumi ya Azerbaijan kuhusu suala la viwango, ni hati ya kwanza iliyosainiwa Jumapili hii kwa kuhudhuriwa na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mwenzake wa Azerbaijan Rais Ilham Aliyev.

Hati ya makubaliano ya ushirikiano wa benki kuu kati ya Iran na Azerbaijan ilisainiwa Jumapili hii pia huko Baku na Magavana wa benki kuu za nchi mbili hizo.

Waziri wa Nyumba na Ujenzi wa Miji wa Iran na Waziri wa Usafirishaji wa Azerbaijan walisaini  hati nyingine za ushirikiano katika sekta ya utalii kati ya Shirika la Bidhaa za Kazi za Mikono na Utalii la Iran  na Shirika husika katika uwanja huo la Azerbaijan. Mwaziri hao pia walisaini  protokali ya  kuasisi korido ya usafirishaji ijulikanayo kwa jina la Korido ya Kaskazini-Kusini.

Wakati huo huo Mahmoud Vaezi Waziri wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano wa Iran na Waziri wa Usafirishaji wa Azerbaijann walisaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya usalama wa kielektroniki.

Naye Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Waziri wa Kilimo wa Azerbaijan walimesaini hati ya ushirikiano katika sekta ya utunzaji mazao na mimea.

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Iran ukibadilishana mawazo na wenzao katika kikao mjini Baku

Rais Hassan Rouhani  wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumapili hii amewasili Baku mji mkuu wa Azerbaijan kwa ziara rasmi nchini humo akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa Iran.

Tags