Iran mstari wa mbele katika kulinda mazingira ya Bahari ya Kaspi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote imekuwa na nafasi athirifu na chanya katika kulinda mazingira ya Bahari ya Kaspi na aina mbalimbali za wanyama, ikiwa ni pamoja na Caspian Seal; mamalia adimu zaidi duniani na viumbe wengine wa baharini.
Iran imekuwa na mchango mkubwa katika kulinda spishi za wanyama wanaopatikana katika Bahari ya Kaspi (Caspian Sea) hasa wale wanaojulilikana kwa jina la "Caspian Seal" ambapo kutekelezwa mpango wa kitaifa na kuanzisha vituo vya msaada na uokoaji, ufuatiliaji wa pwani, na ushirikiano wa kikanda ili kuzuia kutoweka kwa mnyama huyu adimu ni miongoni mwa juhudi za Iran za kuwalinda viumbe hao.
Mamalia hao adimu wa baharini jina la "Caspian Seal" wamewekwa kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya Uhifadhi wa Mazingira ya spishi zilizo hatarini kutoweka (IUCN). Upekee wa kijiografia wa mkoa wa Mazandaran huipelelea spishi hiyo ya thamani kuchagua sehemu ya ufukwe wa Bahari ya Kaspi kwa ajili ya kupita na kama makazi yake ya muda.

Sayyid Mohsen Kazemi-Tabar, Mkuu wa Mazingira ya Baharini katika katika Idara Kuu ya kuhifadhi Mazingira katika mkoa wa Mazandaran ameashiria kuongezeka katika ufukwe wa Bahari ya Kaspi idadi ya mizoga ya mamalia hao adimu zaidi duniani na kusema: "Wameliweka katika ajenda yao ya kazi utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa kuwalinda viumbe hao adimu. Kazem-Tabar ameashiria kuanzishwa sekterariati ya Mpango wa Taifa katika Kitivo cha Elimu cha Tarbiat Modares Noor wa Kuwalinda mamalia hao adimu na kuongeza kuwa: Vituo vitatu vya kuwalinda viumbe hao adimu vimeasisiwa katika wilaya za Tonekabon, Babolsar na Miankaleh.
Mkuu wa Mazingira ya Baharini katika katika Idara Kuu ya kuhifadhi Mazingira katika mkoa wa Mazandaran ameongeza kusema: Tayari kumechukuliwa hatua kuhusu vitendea kazi vya vituo hivyo na hivi karibuni tutashuhudia uzinduzi wa vituo hivyo katika wilaya za mkoa huo. Kazem Tabar ameeleza kuwa: Pamoja na mijadala ya mazingira na umuhimu wa kuwalinda viumbe hawa muhimu wa baharini, masuala ya elimu na kitamaduni pia yamo katika ajenda yao ya kazi.
Iran inasisitiza kuwa kuwalinda mamalia hao adimu kwa jina la Caspian Seal kunahitaji ushirikiano kati ya mataifa ya Kaspi, ikiwa ni pamoja na Russia, Turkmenistan, Kazakhstan na Jamhuri ya Azerbaijan. Ushirikiano huu unaweza kujumuisha ufuatiliaji wa pamoja, upashanaji habari, na hatua zilizoratibiwa za uhifadhi.
Hii ni katika hali mbayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechukua hatua muhimu za kuilinda Bahari ya Kaspi kwa kujiunga na Mkataba wa Tehran na kutekeleza protokali za mazingira. Hatua hizo ni pamoja na kutathmini uharibifu wa mazingira, kutekeleza miradi, kukabiliana na kuchafuliwa mafuta na kufanya jitihada za kulinda maisha ya wanyama na mimea katika eneo.

Mkataba wa Tehran ulipasishwa mwaka 1385 Hijria Shamsia sawa na mwaka 2016 Miladia kati ya nchi tano za pambizoni mwa Bahari ya Kaspi ambazo ni Iran, Russia, Kazakhstan, Jamhuri ya Azerbaijan na Turkimenistan. Mkataba huu una protokali tano kuhusu mazingira ambapo Iran ina mchango mkubwa katika kutekelezwa protokali hizo.
Kwa kuzingatia nafasi yake ya kijiografia, rasilimali za kiuchumi na bayoanuwai; Iran imetoa kipaumbele katika uga wa kikanda na kimataifa kwa suala la kulinda mazingira ya Bahari ya Kaspi. Bahari hii ina mchango muhimu katika usalama wa chakula, ustawi endelevu na usalama wa mfumo ikolojia wa kaskazini mwa nchi.
Iran pia ina ukanda mrefu wa pwani katika mikoa ya Mazandaran, Gilan na Golestan ambayo imeathiriwa moja kwa moja na Bahari ya Kaspi. Hali ya unyevunyevu na hewa kutoka Bahari ya Kaspi imesababisha mazingira ya kijani kibichi, kilimo kinachostawi, na vivutio vya asili kaskazini mwa nchi. Bahari hiyo pia ni chanzo muhimu cha shughuli za uvuvi, mafuta na gesi, usafiri wa baharini na utalii. Kwa iran suala la kuilinda bahari ya Kaspi si tu ni jukumu la kimazingira bali ni mtaji kwa ajili ya vizazi vijavyo ambapo mlingano baina ya uatwasii na mazingira unaweza kudumishwa na kuboreshwa kupitia usimamizi endelevu wa rasilimali.
Iran imekuwa na nafasi kuu na ya uwajibikaji katika kuhifadhi mazingira ya Bahari ya Kaspi. Jitihada hizi si tu ni muhimu kwa ajili ya kulinda maliasili za nchi, mimea na wanyama katika eneo, bali pia zina umuhimu kwa ajili ya ustawi endelevu, kwa usalama wa chakula na ushirikiano wa kikanda.