Iran yalaani mashambulizi ya karibuni ya Israel kusini mwa Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i132126-iran_yalaani_mashambulizi_ya_karibuni_ya_israel_kusini_mwa_lebanon
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulizi ya karibuni ya anga ya Israel kusini mwa Lebanon, na kuzibebesha dhima nchi zilizodhamini makubaliano ya kusitisha vita yaani Ufaransa na Marekani kwa kutoichukulia hatua Israel.
(last modified 2025-10-18T07:49:40+00:00 )
Oct 18, 2025 07:49 UTC
  • Iran yalaani mashambulizi ya karibuni ya Israel kusini mwa Lebanon

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulizi ya karibuni ya anga ya Israel kusini mwa Lebanon, na kuzibebesha dhima nchi zilizodhamini makubaliano ya kusitisha vita yaani Ufaransa na Marekani kwa kutoichukulia hatua Israel.

Esmail Baqaei amesema kuwa mashambulizi ya anga yaliyofanywa jana na Israel kusini mwa Lebanon yanadhihirisha kukiukwa wazi umoja wa ardhi nzima na mamlaka ya kitaifa ya Lebanon uliofanywa na Israel. 

Ameongeza kuwa,  utawala wa Israel unaendelea kukiuka makubaliano ya kusitisha vita kwa miezi kadhaa sasa; ambapo hadi sasa utawala huo umekiuka makubaliano hayo mara 5,000 na kupelekea kujeruhiwa wananchi wa Lebanon, kuharibiwa miundo mbinu na kuvuruga ujenzi na uchumi wa nchi hiyo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa hali hii ya mambo inasabishwa na Ufaransa na Marekani ambazo hazichukui hatua zozote mkabala wa jinai za Israel. 

"Ufaransa na Marekani zinabeba dhima ya moja kwa moja kwa ukiukaji huu tajwa wa makubaliano ya kusimamisha vita unaofanywa na utawala wa Israel," amesema Esmail Baqaei.