Araqchi: Teknolojia haiwezi kuangamizwa kupitia mashambulizi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135304-araqchi_teknolojia_haiwezi_kuangamizwa_kupitia_mashambulizi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran vinavyofanya kazi kwa malengo ya kiraia katika vita vya siku 12 na kusema baadhi ya majengo, taasisi na suhula za nyuklia zinazotumika kwa malengo ya amani za Iran zilidhurika hata hivyo teknolojia haiweza kuangamizwa kupitia mashambulizi.
(last modified 2026-01-10T04:25:13+00:00 )
Jan 10, 2026 04:25 UTC
  • Sayyid Abbas Araqchi
    Sayyid Abbas Araqchi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran vinavyofanya kazi kwa malengo ya kiraia katika vita vya siku 12 na kusema baadhi ya majengo, taasisi na suhula za nyuklia zinazotumika kwa malengo ya amani za Iran zilidhurika hata hivyo teknolojia haiweza kuangamizwa kupitia mashambulizi.

Sayyid Abbas Araqchi amesema katika mahojiano na televisheni ya al Manar kwamba: Hali ya Iran kiujumla ni nzuri ingawa yapo matatizo kutokana na vikwazo na baadhi ya matatizo ya kichumi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: Viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanadai kuwa maajenti wa Shirika la Ujasusi la utawala huo Mossad wapo Tehran na nchini Iran na kwamba wamehusika katika ghasia na machafuko ya karibuni hapa nchini. 

Araqchi amesema: Pande hizo zilikusudia kufanya nchini Iran yale yaliyofanyika huko Venezuela na walidhani kwamba wanaweza kuilazimisha Iran isalimu amri katika muda wa siku tatu lakini wamegonga mwamba. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: Iran iko tayari kufikia makubaliano ya kiadilifu na ya heshima kwa msingi wa kuheshmiana pande mbili lakini haina uhakika kama Wamarekani wanataka kitu kama hicho. 

"Bejamnin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni anazungumzia njozi yake ya Israel Kubwa na kutoa vitisho kwa nchi zote za kanda hii hata hivyo amekumbana na muqawama ngangari huko Lebanon na Iran," amesema Sayyid Abbas Araqchi. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran juzi Alhamisi alifanya ziara huko Beirut mji mkuu wa Lebanon kwa lengo la kudumisha mawasiliano ya kidiplomasia na kuzungumza moja kwa moja na viongozi wa nchi hiyo.