Iran yavunja rekodi ya uzalishaji wa gesi asilia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135618-iran_yavunja_rekodi_ya_uzalishaji_wa_gesi_asilia
Shirika la Taifa la Gesi la Iran limetangaza kuwa, limeweka rekodi mpya ya uzalishaji wa kila siku wa gesi asilia, sambamba na kuongezeka mahitaji ya familia, mitambo ya umeme na matumizi ya viwandani ya nishati hiyo muhimu.
(last modified 2026-01-18T07:03:52+00:00 )
Jan 18, 2026 07:03 UTC
  • Iran yavunja rekodi ya uzalishaji wa gesi asilia

Shirika la Taifa la Gesi la Iran limetangaza kuwa, limeweka rekodi mpya ya uzalishaji wa kila siku wa gesi asilia, sambamba na kuongezeka mahitaji ya familia, mitambo ya umeme na matumizi ya viwandani ya nishati hiyo muhimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Gesi la Iran (NIGC), Saeed Tavakkoli, alisema jana Jumamosi kwamba shirika hilo limefanikiwa kusambaza mitacubic milioni 882 (mcm) za gesi asilia kwenye gridi ya taifa ya umeme tarehe 3 mwezi huu wa Januari, ikionesha rekodi mpya ya uzalishaji wa gesi hiyo ikilinganishwa na siku hiyo mwaka jana.

Tavakkoli ameongeza kuwa, usambazaji wa gesi kwenye mitambo ya umeme ya Iran pia ulikuwa mkubwa na kuweka rekodi mpya ya mitacubic 162.1 kwa siku ikilinganishwa na siku kama hiyo mwaka uliopita.

Amesema kwamba, tangu mwanzo wa mwaka wa Kiiran wa Hijria Shamsia ambao uliingia tarehe 21 Machi, usambazaji wa gesi kwenye mitambo ya umeme uliongezeka kwa mitacubic  bilioni 3.2 nchini Iran. Katika kipindi hicho, gesi iliyosambazwa viwandani ikiwa ni pamoja na viwanda vya kuzalisha saruji na chuma, pia iliongezeka. 

Ripoti hizo zimetolewa huku Iran ikifanikiwa kudhamini mahitaji ya nishati ya wananchi wake, na kuzuia kukatwa umeme wakati wa baridi kali ambao kwa kawaida husababishwa na uhaba wa gesi asilia kwenye mitambo ya umeme.

Tofauti na nchi nyingi duniani ambapo gesi asilia hutumika sana kwa uzalishaji wa umeme, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imehakikisha kwamba, matumizi ya gesi asilia yanatumika kwa upana zaidi na imesambaza gesi hiyo katika nyumba zote za wananchi ambao wanatumia moja kwa moja nishati hiyo majumbani bila ya kuhitaji mitungi ya gesi.