Pezeshkian amhutubu Trump: Wavamizi huja na kwenda, lakini Iran itabaki
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137280-pezeshkian_amhutubu_trump_wavamizi_huja_na_kwenda_lakini_iran_itabaki
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amekosoa vikali vitisho vya kukaririwa vya Rais wa Marekani, Donald Trump kwamba ataisambaratisha Iran, akisiitiza kuwa, wavamizi na waharibifu mithili Trump walikuja na wakaondoka, lakini Iran imeendeelea kubakia.
(last modified 2026-03-11T04:34:37+00:00 )
Mar 11, 2026 04:34 UTC
  • Pezeshkian amhutubu Trump: Wavamizi huja na kwenda, lakini Iran itabaki

Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amekosoa vikali vitisho vya kukaririwa vya Rais wa Marekani, Donald Trump kwamba ataisambaratisha Iran, akisiitiza kuwa, wavamizi na waharibifu mithili Trump walikuja na wakaondoka, lakini Iran imeendeelea kubakia.

Katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa X jana Jumanne, Rais Pezeshkian amebainisha kuwa, hakuna dola au mamlaka iliyofanikiwa kufuta jina kubwa la Iran katika kipindi cha miaka 6,000 ya turathi ya utamaduni wa Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza bayana kuwa, mtu yeyote mwenye kuendekeza wazo hilo la kipumbavu la kuisambaratisha Iran hajui chochote kuhusu historia na tamaduni za kale.

Hapo jana pia, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran alitoa onyo kali akijibu vitisho vipya vilivyotolewa na Trump vya kuwashambulia na kuwaua wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Ali Larijani alisema katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa X Jumanne kuwa, taifa la Iran haliogopi vitisho hewa vya maadui, akimuonya Trump kwamba yumkini yeye ndiye atakayetokomezwa.

Kabla ya hapo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema vitisho hivyo vipya vilivyotolewa na Trump dhidi ya wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ni kukiri wazi wazi kwa kiongozi huyo wa Marekani juu ya kufanya jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu.