Kamanda: ‘Baba wa Makombora ya Iran’ tayari kushambulia ngome za adui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i142304-kamanda_baba_wa_makombora_ya_iran’_tayari_kushambulia_ngome_za_adui
Mshauri mwandamizi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kwamba iwapo adui atafanya mahesabu yoyote mabaya dhidi ya Iran, kombora ambalo amelitaja kuwa “baba wa makombora ya Iran” liko tayarikusambaratisha miundombinu yake ya nishati pamoja na uwekezaji wake kote katika eneo hili.
(last modified 2026-10-19T10:28:29+00:00 )
Oct 19, 2026 10:27 UTC
  • Mkombora ya Zulfaqar ya Iran
    Mkombora ya Zulfaqar ya Iran

Mshauri mwandamizi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kwamba iwapo adui atafanya mahesabu yoyote mabaya dhidi ya Iran, kombora ambalo amelitaja kuwa “baba wa makombora ya Iran” liko tayarikusambaratisha miundombinu yake ya nishati pamoja na uwekezaji wake kote katika eneo hili.

Brigedia Jenerali Mohammad Reza Naqdi, mshauri mwandamizi wa Kamanda Mkuu wa IRGC, alitoa kauli hiyo siku ya Jumapili akihutubia maelfu ya washiriki katika kongamano la kampeni ya “Kujitolea kwa Ajili ya Iran” (Fadakari baraye Iran) katika mji wa kaskazini wa Sari.

Kauli hiyo ya “baba wa makombora” ilikuwa jibu la wazi la kimtazamo na kishujaa dhidi ya tishio la wazi la Rais wa Marekani Donald Trump la kutaka kutumia bomu zito la GBU-43/B, linalojulikana kama “mama wa mabomu yote”, dhidi ya miundombinu ya nishati na vituo vya nyuklia vya Iran.

Ameongeza kuwa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameonyesha uwezo wa juu wa makombora na nguvu kubwa ya kuzuia uchokozi (deterrence) katika kukabiliana na vitisho vya kijeshi vya Marekani, jambo linaloyapa uwezo wa kutoa jibu madhubuti na la maamuzi kwa chokochoko yoyote ile.

Jenerali Naqdi amesisitiza kuwa uwezo na ushindi wa Iran kimsingi hautokani na zana za kijeshi pekee, bali unatokana na uwepo thabiti, muamko na utayari wa dhati wa wananchi wa Iran katika nyanja zote.

Kamanda huyo wa IRGC alisema kuwa utayari na kusimama kidete kwa taifa kumezuia uvamizi wa ardhini na kuyalazimu manowari na meli za kivita za maadui kurudi nyuma kwa umbali wa kilomita 1,000 baharini.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Jenerali Naqdi alisema kauli za hivi karibuni za Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kuishiwa na subira na kutishia kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya Iran ni “ukiri wa wazi wa kushindwa” mbele ya kusimama imara kwa wananchi wa Iran.

Aliongeza kuwa matamshi hayo yanakinzana waziwazi na madai ya Washington ya kupata ushindi, akibainisha kuwa upande unaodai kushinda hauwezi kulalamika kuwa subira yake imefikia kikomo.

Akijibu vitisho vya Marekani vinavyohusisha silaha za kisasa, ikiwemo hilo “mama wa mabomu yote,” kamanda huyo wa IRGC amesema mabomu yenye uzito wa tani 14 yalirushwa nchini Iran wakati wa vita vya siku 12, lakini baadhi yake hayakulipuka na hatimaye yakadhibitiwa na kutwaliwa na vikosi vya Iran.

Alieleza kuwa hivi sasa Iran inamiliki taarifa za siri za silaha hizo na iko mbioni kuziunda.

Uwezekano wa Marekani kutumia bomu hilo kubwa zaidi lisilo la nyuklia katika ghala lake la silaha ni ishar ya kupanuka zaidi na kwa kiwango cha hatari vita kati ya Iran na Marekani.

Katika ujumbe wake siku ya Jumapili, Msemaji wa IRGC, Brigedia Jenerali Hossein Mohebi, alisema ni “ustaarabu wa kishenzi na kinyama” pekee unaoweza kutumia neno tukufu la “Mama” kubatiza bomu lake zito zaidi lenye kuangamiza watu.