Iran yalaani miripuko ya kigaidi huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i14728-iran_yalaani_miripuko_ya_kigaidi_huko_syria
Bahram Qassemi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na magaidi watenda jinai wa kitakfiri na waungaji mkono wao wa Kiwahabi kwa kuwalenga raia wasio na hatia huko Syria, vinaonyesha kutokuwa na uwezo na kushindwa magaidi hao katika mapambano ya kijeshi na jinsi walivyo na ndoto tupu za kisiasa katika eneo hili.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 06, 2016 03:03 UTC
  • Iran yalaani miripuko ya kigaidi huko Syria

Bahram Qassemi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na magaidi watenda jinai wa kitakfiri na waungaji mkono wao wa Kiwahabi kwa kuwalenga raia wasio na hatia huko Syria, vinaonyesha kutokuwa na uwezo na kushindwa magaidi hao katika mapambano ya kijeshi na jinsi walivyo na ndoto tupu za kisiasa katika eneo hili.

Bahram Qassemi amelaani mashambulio kadhaa ya kigaidi yaliyojiri katika maeneo tofauti huko Syria na mikoa ya Tartous, Homs, Hasaka na huko Damascus na kusababisha vifo vya makumi ya raia wa nchi hiyo wasio na hatia na kutoa mkono wa pole kwa serikali na wananchi wa Syria.

Miripuko ya mabomu kwa wakati mmoja iliyotokea katika maeneo ya Homs, Tartous na Hasaka huko Syria

Qassemi ameongeza kuwa kitendo cha magaidi watenda jinai wa kitakfiri na waungaji mkono wao wa Kiwahabi cha kuwalenga kwa mashambulizi raia wa Syria wasio na hatia, kinaonyesha kutokuwa na uwezo na kushindwa magaidi hao katika mapambano ya kijeshi na kinadhiihrisha jinsi magaidi hao walivyo na ndoto tupu za kisiasa katika eneo hili; kunakopelekea kukaririwa kila uchao jinai za kutisha kama hizo na kusababisha matukio ya kuhuzunisha na kufedhehesha huko Syria, Iraq na Yemen.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, taasisi za kimataifa zinapasa kutekeleza vizuri majukumu yao ya kihistoria, kisheria na kibinadamu kwa azma thabiti katika kukabiliana na ugaidi wa kitakfiri.