Iran yakosoa waraka wa Bunge la Umoja wa Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i16984-iran_yakosoa_waraka_wa_bunge_la_umoja_wa_ulaya
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa waraka ambao utachunguzwa na Bunge la Umoja wa Ulaya kuhusu mustakabali wa uhusiano wa umoja huo na Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 08, 2016 04:45 UTC
  • Iran yakosoa waraka wa Bunge la Umoja wa Ulaya

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa waraka ambao utachunguzwa na Bunge la Umoja wa Ulaya kuhusu mustakabali wa uhusiano wa umoja huo na Iran.

Katika taarifa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi amesema baadhi ya sehemu za waraka huo si sahihi na kwamba ni jambo linalotilia shaka kuwa zimewekwa katika waraka huo. Qassemi amesema waraka huo wenye anwani ya, "Strategia ya EU Kuhusu Iran Baada ya Mapatano ya Nyuklia", una nukta chanya na baadhi ya nukta ambazo hazina msingi wowote. Amesema ingawa nukta chanya za waraka huo zinaleta matumani katika uimarishwaji uhusiano wa Iran na EU lakini nukta zinazohusu hali ya haki za binadamu nchini Iran hazijazingatia uhalisia wa mambo na zimetayarishwa kwa kutegemea kampeni na propaganda chafu za wanaoipinga Iran.

Amesema pamoja na kuwa mazungumzo kuhusu haki za binadamu baina ya Iran na Umoja wa Ulaya yatafanyika katika siku za usoni, kuwepo nukta kama hizo hakutasaidii kuimarisha mazungumzo kuhusu haki za binadamu bali kunatia nguvu ile kauli kuwa umoja huo unaingilia mambo ya ndani ya Iran.

Waraka huo unatazamiwa kupigiwa kura Alhamisi ijayo ambapo imetabiriwa kuwa, Umoja wa Ulaya utaanzisha tena uhusiano wa kawaida na Iran baada ya kufikiwa mapatano ya nyuklia Julai 2015 baina ya Tehran na madola sita makubwa duniani.