Larijani: Uchaguzi wa Bunge umezidisha hadhi ya Iran kimataifa
(last modified Mon, 29 Feb 2016 08:17:19 GMT )
Feb 29, 2016 08:17 UTC
  • Larijani: Uchaguzi wa Bunge umezidisha hadhi ya Iran kimataifa

Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iran katika uchaguzi uliofanyika Ijumaa iliyopita hapa nchini yamezidisha hadhi ya Iran katika nyanja za kimataifa.

Dakta Ali Larijani amesema mapema leo katika kikao cha wazi cha kwanza cha Bunge baada ya uchaguzi wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Kiislamu na wa 5 wa Baraza la Wataalamu kwamba mahudhurio makubwa ya Wairani katika chaguzi hizo yameonesha usalama na amani ya hali ya juu hapa nchini na kupeleka juu zaidi hadhi ya nchi hii kimataifa.

Dakta Larijani amesema Iran ni miongoni mwa nchi chache katika eneo la Mashariki ya Kati zenye demokrasia halisi. Ameongesza kuwa mahudhurio makubwa ya wananchi katika chaguzi hizo yametoa ujumbe kwa nchi zote kwamba Jamhuri ya Kiislamu inaungwa mkono na wananchi na kwamba taifa la Iran liko tayari kwa ajili ya harakati mpya ya ustawi na maendeleo na kujenga Iran ya Kiislamu, huru na inayojitawala.

Chaguzi za Bunge na Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Iran zilifanyika Ijumaa iliyopita kote nchini.

Tags