Jun 09, 2017 08:21 UTC
  • Wairan wawaaga mashahidi wa mashambulizi ya kigaidi ya Tehran

Shughuli ya kuwaaga mashahidi wa mashambulizi ya juzi hapa Tehran imefanyika kwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu pamoja na familia za mashahidi hao katika ukumbi wa Aftab wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge.

Hujjatul Islam wal Muslimin Muhammad Muhammadi Golepaighani Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, baadhi ya mawaziri, wabunge na familia za mashahidi waliouliwa wameshiriki katika shughuli hiyo leo hii.

Spika wa Bunge la Iran, Dakta Ali Larijani amehutubia watu walioshiiki kwenye shughuli hiyo iliyoendelea kwa muda wa masaa mawili ya kuwaaga mashahidi wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika juzi hapa Tehran. 

Viongozi wa serikali katika marasimu ya kuwaaga mashahidi wa mashambulizi ya kigaidi ya Tehran

Miili ya mashahidi imepelekwa katika uwanja wa Swala ya Ijumaa katika Chuo Kikuu cha Tehran kwa ajili ya taratibu za maziko. Magaidi wa kundi la Daesh juzi Jumatano tarehe 7 Juni walifanya mashambulizi mawili ya kigaidi katika Haram Tukufu la Imamu Khomeini (MA) na katika jengo la Bunge la Iran mjini Tehran. Askari usalama wa Iran walifanikiwa kuwaangamiza magaidi wote na kumtia nguvuni mmoja wao. Watu 17 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi hayo ya kigaidi. 

Tags