Rais wa Iran asisitiza nafasi muhimu ya wanawake katika maendeleo ya jamii
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i30940-rais_wa_iran_asisitiza_nafasi_muhimu_ya_wanawake_katika_maendeleo_ya_jamii
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza nafasi muhimu ya wanawake katika ustawi na maendeleo ya jamii sambamba na kusukuma mbele gurudumu la malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2017 03:48 UTC
  • Rais wa Iran asisitiza nafasi muhimu ya wanawake katika maendeleo ya jamii

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza nafasi muhimu ya wanawake katika ustawi na maendeleo ya jamii sambamba na kusukuma mbele gurudumu la malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Rais Rouhani sambamba na kuashiria mahudhurio ya wanawake katika nyanja mbalimbali za kielimu amebainisha kwamba, hii leo wanawake wako bega kwa bega na wanaume katika nyuga zote.

Rais Rouhani sambamba na kusisitiza kwamba, hii leo walimwengu wanapaswa kudiriki ukweli na uhakika katika dunia ya leo na Uislamu amebainisha kwamba, wanawake ili waweze kuwa na mahudhurio katika nyanja mbalimbali za uongozi wanapaswa kufanywa hima na juhudi zaidi kama ambavyo hii leo wana mchango mkubwa katika masuala ya kiutafiti, kisiasa na kijamii.

Rais Hassan Rouhani katika picha ya pamoja na wanaharakati wa masuala ya wanawake na familia

Amesema, serikali yake inafanya juhudi za kutoa fursa sawa kwa wanawake na wanaume na kubainisha kwamba, maendeleo ya kimaada na kimaanawi ni mdaiwa wa uweko heshima na kila mmoja kumheshimu mwenzake katika jamii.

Aidha Rais wa Iran ameonghezaa kuwa, katika jamii kuna haja ya kila mtu kuheshimu mtazamo wa mwenzake.

Rais Hassan Rouhani akizungumza mbele ya wanaharakati wa masuala ya wanawake na familia ameashiria kuongezeka idadi ya Wabunge wanawake katika Bunge la 10 la Iran, na hata kwenye Mabaraza ya Kiislamu ya Miji na Vijiji na kubainisha kwamba, wanawake kwa kuufanya hima na bidii wanaweza kuwa viongozi na wasimamizi wa masuala mbalimbali katika jamii.