Marekani ina ndoto ya kijinga ya kuuangusha mfumo wa Kiislamu Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i31752-marekani_ina_ndoto_ya_kijinga_ya_kuuangusha_mfumo_wa_kiislamu_iran
Kamanda wa ngazi za juu nchini Iran amepuuzilia mbali matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani aliyasema Washington inataka kuuangusha mfumo wa Kiislamu wa Iran na kusema hiyo ni 'ndoto ya kijinga'.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Jul 14, 2017 03:18 UTC
  • Marekani ina ndoto ya kijinga ya kuuangusha mfumo wa Kiislamu Iran

Kamanda wa ngazi za juu nchini Iran amepuuzilia mbali matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani aliyasema Washington inataka kuuangusha mfumo wa Kiislamu wa Iran na kusema hiyo ni 'ndoto ya kijinga'.

Naibu Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Masoud Jazayeri amesema Iran haibabaishwi na matamshi kama hayo.

Ameongeza kuwa: "Ndoto ya Wamarekani kuhusu kuuangusha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran si kingine ila ni ndoto za kijinga ambazo hazitubabaishi."

Jazayeri bila kufafanua zaidi amesema Iran itajibu kivitendo matamshi hayo ya kipuuzi ya Wamarekani.

Hivi karibuni Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis alidai kuwa eti Iran si nchi ya kidemokrasia na kwamba Washington inapanga kuuangusha mfumo wa Kiislamu unaotawala nchini Iran.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis

Jazayeri amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejiwekea malengo na sera maalumu na itaendelea kuyatimua madola ajinabi yanayokuja katika eneo na wala haitaterereka katika msimamo wako huo mtakatifu.

Hali kadhalika Naibu Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran na ksuema Tehran imeandaa mipango ambayo itaidhuru vikali Marekani.