Aug 16, 2017 04:02 UTC
  • Larijani apongeza ushindi wa Hizbullah ya Lebanon katika vita vya siku 33

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ametuma ujumbe tofauti kwa Nabih Berri Spika wa Bunge la Lebanon na Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya nchi hiyo kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Lebanon katika vita vya siku 33.

Vita vya siku 33 kati ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel na wanamapambano wa Hizbullah vilianza mwezi Julai mwaka 2006 na kumalizka tarehe 14 Agosti mwaka huo kwa kupata ushindi harakati ya Hizbullah.

Utawala wa Kizayuni ulilazimika kusalimu amri katika vita hivyo kufuatia kipigo na hasara kubwa uliopata kutoka kwa wanamapambano wa Hizbullah. 

Wanamapambano wa Hizbullah ya Lebanon  

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran jana alimtumia ujumbe Nabih Berri Spika mwenzake wa Lebanon na kueleza kuwa, hakuna shaka kwamba ushindi huo wa fakhari uliopatikana chini ya kivuli cha rehma na baraka za Mwenyezi Mungu, mshikamano na umoja wa wananchi na viongozi wa serikali na wapiganaji shupavu wa Hizbullah waliosabilia nafsi zao  ni fakhari kwa nchi za Kiislamu na jambo la kuvunja moyo kwa utawala haramu na ghasibu wa Israel.  

Katika ujumbe aliomtumia pia Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameashiria stratejia madhubuti ya kiongozi huyo na kusema kuwa ushindi huo wa mashijaa wa Hizhullah umesajiliwa katika historia ya harakati hiyo ya Kiislamu.

Vijana wa Hizbullah

Dakta Larijani amesema ushindi wa Hizbullah mbali na kuwa ulikuwa fahari na heshima kubwa kwa Lebanon, vilevile umefungua ukurasa mpya katika historia ya mapambano ya mataifa ya Waislamu dhidi ya wavamizi wa Wazayuni na waitifaki wao.

Tags