Ujumbe Muhimu wa Zarif kuhusu mapatano ya nyuklia ya Iran + VIDEO
Katika Ujumbe wake wa video hapo jana Alkhamisi, Muhammad Jawad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa kuna chaguo moja tu la kufanikisha makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita kubwa za dunia, nalo ni Marekani kutekeleza ahadi zake zote kuhusiana na makubaliano hayo.
Huku akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama imara mbele ya kiburi cha Marekani, Zarif amesema kuwa nchi hiyo ya Magharibi haiwezi kufikia mapatano mapya kwa kupiga makelele au kupitia vitisho. Mkuu huyo wa chombo cha diplomasia cha Iran amesema kuwa kamwe Iran hautaweka usalama wake mikononi mwa nchi za kigeni, kufanya mazungumzo mapya juu mapatano ambayo imekuwa ikiyatekeleza kwa nia njema au kuongeza jambo jingine jipya kwenye mapatano hayo.