Maonyesho ya 23 ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi nchini Iran
Maonyesho ya 23 ya Kimataifa ya Mafuta, Gesi, Usafishaji na Petrokemikali yanatazamiwa kuanza kesho Jumapili hapa mjini Tehran.
Maonyesho hayo ambayo ni makubwa zaidi ya kibiashara na kiviwanda nchini katika sketa ya mafuta, hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na mashirika makubwa ya kitaifa na kimataifa.
Moja kati ya malengo ya maonyesho hayo ni kuonyesha mafanikio ya hivi karibuni katika sekta za mafuta na gesi sambamba na kuimarisha ushirikiano na nchi pamoja na mashirika mbali mbali katika sekta hiyo muhimu.
Aidha maonyesho hayo hutumika katika kuimarisha uwezo wa sekta ya mafuta na gesi nchini Iran kupitia ubadilishanaji uzoefu na mashirika ya kimataia.
Kati ya yatakayoonyeshwa katika maonyesho ya mwaka huu ni vifaa vipya vya utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi, uundwaji mabomba, viwanda vya usafishaji mafuta na mbinu za kisasa za usafirishaji mafuta.