Rais Rouhani: Wanaolitakia mabaya taifa la Iran muda si mrefu watasailimu amri
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46420-rais_rouhani_wanaolitakia_mabaya_taifa_la_iran_muda_si_mrefu_watasailimu_amri
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kuna haja ya kukabiliana na vitisho vya adui na kuvibadilisha kuwa fursa, kwani wanaolitakia mabaya taifa hili muda si mrefu watasalimu amri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 28, 2018 09:06 UTC
  • Rais Rouhani: Wanaolitakia mabaya taifa la Iran muda si mrefu watasailimu amri

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kuna haja ya kukabiliana na vitisho vya adui na kuvibadilisha kuwa fursa, kwani wanaolitakia mabaya taifa hili muda si mrefu watasalimu amri.

Rais Rouhani amesema hayo katika hafla ya ufunguzi wa hatua ya pili ya mradi wa gesi wa Nyota ya Ghuba ya Uajemi (Setareh Ghalij Fars) huko Bandar Abbas kusini mwa Iran na kubainisha kwamba, zama hizi ni kipindi muhimuu cha historia ambapo kuna haja ya kusimama na kupambana na adui na wakati huo huo kuvibadilisha vitisho vya adui na kuvifanya kuwa fursa.

Rais Rouhani amesema kuwa, vikwazo na mashinikizo ni fursa kwa ajili ya ubunifu na kuchanua vipaji vya uzalishaji na hivyo kuweza kukabiliana na madola ya kibeberu duniani. 

Rais Hassan Rouhani

Aidha Dakta Rohani ameongeza kuwa, usalama na nafasi ya kiistratejia ya Iran ni muhimu mno na tukilinganisha nafasi ya sasa ya Iran na ya baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati na hata baadhi ya nchi za kusini mwa Ghuba ya Uajemi tunaweza kuona jinsi taifa hili lilivyo katika nafasi na mazingira bora.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, taifa hili limesimama imara na kwamba, bila shaka litamshinda adui, kwani irada na uimara wa wananchi wa taifa hili umemchosha adui na muda si mrefu atasalimu amri.