Rouhani: Iran ndiyo mhanga mkubwa zaidi wa ugaidi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50033-rouhani_iran_ndiyo_mhanga_mkubwa_zaidi_wa_ugaidi_duniani
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mashambulizi ya kigaidi hayawezi kuzima azma kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya kupambana kwa nguvu zote na ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 08, 2018 06:13 UTC
  • Rais Hassan Rouhani
    Rais Hassan Rouhani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mashambulizi ya kigaidi hayawezi kuzima azma kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya kupambana kwa nguvu zote na ugaidi.

Rais Rouhani ameyasema hayo mapema leo katika ufunguzi wa mkutano wa pili maspika wa nchi sita za kanda hii unofanyika mjini Tehran na kuongeza kuwa, tangu mwanzoni mwa kuasisiwa kwake, Jamhuri ya Kiislamu imekuwa ikikabiliwa na uovu huo, na mashambulizi hayo ya kigaidi yamesababisha hasara kubwa ya nafsi na mali.

Rais Rouhani amesema mashambulizi ya kigaidi na utegaji wa mabomu wa miaka ya 1981 na mauaji ya zaidi ya raia elfu 17 wa kawaida nchini Iran katika kipindi chote cha miaka 40 iliyopita vilivyofanywa na makundi ya kigaidi yanayopewa hifadhi katika nchi za Magharibi ni sehemu ya hasara hiyo kubwa iliyosababishwa na magaidi nchini Iran.

Mkutano wa maspika wa mabunge ya nchi 6, Tehran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ameyataja mauaji ya wasomi wa nyuklia wa Iran yaliyofanywa na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za Magharibi mwanzoni mwa muongo huu, shambulizi la kundi la kigaidi la Daesh dhidi ya jengo la Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) mwaka jana wa 2017, shambulizi la kigaidi la hivi karibuni katika mji wa Ahvaz kusini magharibi mwa Iran na vilevile shambulizi ya siku chache zilizopita katika eneo la Cahabahar kusini magharibi mwa Iran kuwa ni sehemu ya hasara na madhara makubwa yaliyosababishwa na ugaidi.

Rais Rouhani ametoa pendekezo lenye viapengee 8 la kujenga eneo imara. Amesema: Tehran iko tayari kushiriki ipasavyo katika ujenzi wa eneo hilo.

Amesema: "Nchi iliyoanzisha vita vya kibiashara dhidi ya China, inayoiumiza Pakistan, inayoidhalilisha Afganistan, inayoiadhibu Uturuki, inayotoa vitisho dhidi ya Russia na kuiwekea vikwazo Iran ndiye mtuhumiwa mkubwa zaidi wa kukanyanga sheria na makubaliano ya kimataifa; na sisi tutasimama kidete mbele ya Marekani."

Mkutano wa Tehran unahudhuriwa na maspika wa mabunge ya Iran, China, Russia, Uturuki, Pakistan na Afghanistan