Russia yasisitiza kushirikiana na Iran katika sekta ya nishati ya nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i51732-russia_yasisitiza_kushirikiana_na_iran_katika_sekta_ya_nishati_ya_nyuklia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametangaza kuwa, Moscow itaendelea kushirikiana kwa pande zote na Iran ikiwa ni pamoja na katika sekta ya nishati ya nyuklia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 23, 2019 00:14 UTC
  •  Russia yasisitiza kushirikiana na Iran katika sekta ya nishati ya nyuklia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametangaza kuwa, Moscow itaendelea kushirikiana kwa pande zote na Iran ikiwa ni pamoja na katika sekta ya nishati ya nyuklia.

Maria Zakharova amesema kuwa vitisho vya Washington kwamba itaiwekea vikwazo sekta ya biashara ya Russia kutokana na nchi hiyo kushirikiana na Iran hazikubaliki na zinatia wasiwasi. Zakharova ameongeza kuwa, jitihada zinazofanywa na Marekani za kuweka mashinikizo na kuitishia sekta ya nishati ya Russia ni mwendelezo wa hatua zisizofaa za serikali ya sasa ya Marekani. 

Ikulu ya Marekani na vitisho vyake dhidi ya sekta ya nishati ya Russia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa viongozi wa Washington wamepoteza mwelekeo na hawazingatii uhakika wa mambo katika hatua zao dhidi ya Iran.

Licha ya hatua hizo dhidi ya Iran za viongozi wa White House, Russia, China na nchi za Ulaya zimetangaza kuwa, ziko tayari kupanua mashirikiano yao ya kiuchumi na Iran. Viongozi wa nchi za Ulaya pia wametangaza kuwa wako tayari kupanua ushirikiano wa kiuchumi na Iran licha ya vitisho hivyo vya ikulu ya Rais wa Marekani.