Waziri wa Ulinzi: Iran inajiimarisha kiulinzi ili kuzima uchokozi wa maadui
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uwezo wa kiulinzi wa nchi hii utaendelezwa na kupanuliwa zaidi na kwa kasi kwa shabaha ya kuzuia chokochoko za maadui.
Brigedia Jenerali Amir Hatami aliyasema hayo jana akihutubia mkutano wa kimataifa wa masuala ya kibinadamu hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, maadui wameanzisha vita vya kiuchumi vya kila upande dhidi ya mfumo wa Kiislamu na nguvu ya kiulinzi ya taifa hili.
Huku akiashiria kuhusu vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran kati ya mwaka 1980 na 1988, Waziri wa Ulinzi wa Iran ameeleza kuwa, "Zaidi ya hektari milioni 4.8 za ardhi ya Iran zilikuwa zimeejaa mabomu ya kutegwa ardhini. Mabomu hayo alikabidhiwa dikteta Saddam Hussein na wale wanaojinadi na kujipiga kifua kuwa ni watetezi wa haki za binadamu."
Brigedia Jenerali Hatami amesema katu Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu jambo hilo lifanyike tena na kusisitiza kuwa, kudhoofisha nguvu ya kiulinzi ya Iran ni lengo kuu linalofuatiliwa na maadui wa taifa hili.
Ameongeza kuwa, "Kile wanachotuambia leo hii, ni kwamba tusiwe na makombora na tusijiimarishe kiulinzi, katika hali ambayo wanaziruhusu nchi nyingine za eneo hili zirundike silaha na mabomu."
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, ni kwa kuzingatia ukweli huo, ndio maana maadui wanapinga vikali uwezo wa makombora wa Iran pamoja na taifa hili kuwa na nguvu katika Mashariki ya Kati,