Droni ya ujasusi ya Marekani yatunguliwa katika pwani ya kusini mwa Iran
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kutungua drone au ndege isiyo na rubani ya kijasusi ya Marekani ambayo ilikuwa imejipenyeza katika mipaka ya Iran mkoani Hormozgan kusini mwa nchi.
Katika taarifa mapema Alhamisi, IRGC imesema drone ya kijasusi ya Marekani aina ya Global Hawk imetunguliwa karibu na Kouh-e-Mobarak katika eneo la Jask baada ya kukiuka anga ya Iran. Drone ya kijasusi ya RQ-4 Global Hawk ni kati ya ndege za kisasa kabisa za kijasusi za Jeshi la Marekani.
Kampuni inayozalisha aina hii ya ndege zisizo na rubani ya Northrop Grumman imesema kuwa droni hizi zina uwezo wa kuruka katika anga za juu zaidi kwa muda wa masaa zaidi ya 30 huku zikichukua picha nzuri za maeneo makubwa ya ardhi katika hali zote za hewa.
Taarifa zaidi kuhusu kutungulia ndege hiyo ya kijasusi ya Marekani zitatolewa baadaye.