Zarif: Iran inafanya mazungumzo na nchi mbalimbali kuhusu makubaliano ya kifedha
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54297-zarif_iran_inafanya_mazungumzo_na_nchi_mbalimbali_kuhusu_makubaliano_ya_kifedha
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Tehran inafanya mazungumzo na nchi mbalimbali ili kufikia makubaliano ya kifedha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 23, 2019 03:18 UTC
  • Zarif: Iran inafanya mazungumzo na nchi mbalimbali kuhusu makubaliano ya kifedha

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Tehran inafanya mazungumzo na nchi mbalimbali ili kufikia makubaliano ya kifedha.

Muhammad Javad Zarif amesema kuwa hadi kufikia sasa Iran imeshafanya mazungumzo kuhusu suala hilo na Uturuki, Russia, China, Jamhuri ya Azerbaijan na nchi nyingine mbalimbali na imeshafikia makubaliano na baadhi ya nchi kuhusu suala hilo. Zarif ameongeza kuwa Iran imefanya juhudi zake zote ili kukabiliana na vikwazo vya Marekani.

Rais Donald Trump wa Marekani tarehe Nane Mei mwaka huu alikiuka makubaliano ya nyuklia ya JCPOA alipotangaza uamuzi wa upande mmoja na kujitoa kwenye makubaliano hayo ya kimataifa na kisha kutangaza kuvirejesha vikwazo vya nyuklia dhidi ya Iran. Hatua hiyo ya Trump imekosolewa na kupingwa pakubwa ndani ya Marekani kwenyewe na katika uga wa kimataifa.