Mousavi: Iran inajibu diplomasia kwa diplomasia na mashinikizo kwa muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54463-mousavi_iran_inajibu_diplomasia_kwa_diplomasia_na_mashinikizo_kwa_muqawama
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi ya uropokojaji ya hivi karibuni ya viongozi wa Marekani khususan Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la nchi hiyo aliyesema kuwa Iran inapasa kujibu diplomasia kwa diplomasia kwa kusema: Iran inajibu diplomasia kwa diplomasia na mashinikizo kwa muqawama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 30, 2019 08:23 UTC
  • Mousavi: Iran inajibu diplomasia kwa diplomasia na mashinikizo kwa muqawama

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi ya uropokojaji ya hivi karibuni ya viongozi wa Marekani khususan Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la nchi hiyo aliyesema kuwa Iran inapasa kujibu diplomasia kwa diplomasia kwa kusema: Iran inajibu diplomasia kwa diplomasia na mashinikizo kwa muqawama.

Sayyid Abbas Mousavi ameeleza kuwa katika kamusi ya serikali ya Marekani neno diplomasia lina maana ya vikwazo na ugaidi wa kiuchumi na kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna jambo lolote lililoshuhudiwa likijibiwa na serikali ya Marekani ghairi ya vikwazo vilivyo kinyume cha sheria, vita na ugaidi wa kiuchumi. Garret Marquis Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani jana alitoa matamshi ya kijuba akitaka kusimamishwa kikamilifu miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani. 

Garrett Marquis aidha ameyataja madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba yuko tayari kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni udiplomasia; na kusisitiza kuwa Tehran inapasa kujibu takwa la Trump la udiplomasia kwa udiplomasia. Baada ya kujitoa kinyume cha sheria katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA,  Rais wa Marekani amejaribu kutumia mbinu mbaimbali kuishawishi Iran kufanya mazungumzo. 

Akizungumza Jumatano iliyopita mbele ya hadhara ya mkuu, maafisa,  majaji na wafanyakazi wa chombo cha mahakama cha Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei alisema: Lengo kuu la pendekezo la Marekani kuhusu kufanya mazungumzo na Iran ni kutaka kulipokonya silaha taifa hili na kulipora njia zinazolifanya kuwa imara. Hivyo wanataka kutumia mazungumzo kulipokonya taifa la Iran silaha na njia zake hizo zinazolifanya kuwa imara ili baada ya hapo walisababishie taifa letu kila balaa wanayoijua. 

Kiongozi Muadhamu katika mkutano na mkuu, maafisa na wafanyakazi wa chombo cha mahakama cha Iran