Meja Jenerali Safavi: Iran ya Kiislamu ni nguvu isiyoweza kushindwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54984-meja_jenerali_safavi_iran_ya_kiislamu_ni_nguvu_isiyoweza_kushindwa
Msaidizi na Mshauri wa ngazi za juu wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran ameeleza kuwa uwezo wa Iran ya Kiislamu unaongezeka siku baada ya siku na kwamba nguvu ya Marekani na Wazayuni inazidi kupungua.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 25, 2019 06:42 UTC
  • Meja Jenerali Safavi: Iran ya Kiislamu ni nguvu isiyoweza kushindwa

Msaidizi na Mshauri wa ngazi za juu wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran ameeleza kuwa uwezo wa Iran ya Kiislamu unaongezeka siku baada ya siku na kwamba nguvu ya Marekani na Wazayuni inazidi kupungua.

Meja Jenerali Sayyid Yahya Rahim Safavi amesema leo katika marasimu ya kukumbuka ya oparesheni ya Mirsad iliyotekelezwa Julai 27 mwaka 1988 kuwa, Iran ni nguvu kubwa isiyoweza kushindwa na kwamba mjadala kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu unashika kasi kuanzia bahari ya Pacific hadi Mediterania  na kwamba Wamarekani wanalazimika kuondoka katika eneo hili.  

Msaidizi na Mshauri wa ngazi ya juu wa Amirijeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran amesema kuwa Marekani ilikuwa nyuma ya pazia la oparesheni iliyoshindwa ya kundi la kigaidi la Munafiqeen magharibi mwa Iran na kuongeza kuwa: Viongozi wa Marekani walitekeleza njama ya oparesheni ya Mirsad kwa kulitumia kundi la Munafiqeen ili kuupindua mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu baaada ya kushindwa mtawalia mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na katika vita vya kulazimishwa vya miaka minane. 

Meja Jenerali Safavi amebainisha kuwa asilimia 80 ya wanachama wa kundi la kigaidi la Munafiqeen waliangamizwa katika oparesheni ya Mirsad; na wengine wakakimbia. Amesema oparesheni hiyo ilikuwa fakhari kwa Wairani na pigo kubwa kwa Wamarekani na kundi la Munafiqeen.  

Hasara na maafa ya adui katika oparesheni ya Mirsad