Zarif: Iran haitasita kulinda usalama wake katika Ghuba ya Uajemi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ghuba ya Uajemi ni kipaumbele cha kwanza kwa usalama wa taifa la Iran na mesisitiza kuwa Iran haitasita katika kulinda usalama wake katika Ghuba ya Uajemi.
Katika ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Twitter Ijumaa, Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Ghuba ya Uajemi ni eneo muhimu sana na kuongeza kuwa, kwa muda mrefu sasa Iran imekuwa ikidhamini usalama wa usafiri wa baharini katika eneo hilo.
Zarif amesema vikosi vya madola ajinabi katika eneo la Ghuba ya Uajemi ni chanzo cha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Ikumbukwe kuwa katika miezi ya hivi karibuni, kwa lengo la kushadidisha mashinikizo dhidi ya Iran, Marekani imeongeza kiwango cha zana zake za kivita katika eneo la Ghuba ya Uajemi na ikishirikiana na waitifaki wake hasa Uingereza imekuwa ikitekeleza hatua za kichochezi.
Marekani imetangaza kuwa, inalenga kuunda muungano mpya wa kijeshi katika eneo la Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kukabiliana na Iran.