Rais Rouhani awatumia salamu za Idi viongozi wa nchi za Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55319-rais_rouhani_awatumia_salamu_za_idi_viongozi_wa_nchi_za_kiislamu
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe viongozi wa nchi za Kiislamu akiwapa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaaba wa kuadhimisha sikukuu ya Idul Adh'ha.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Aug 11, 2019 14:14 UTC
  • Rais Rouhani awatumia salamu za Idi viongozi wa nchi za Kiislamu

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe viongozi wa nchi za Kiislamu akiwapa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaaba wa kuadhimisha sikukuu ya Idul Adh'ha.

Katika ujumbe huo Rais Rouhani amewapongeza Waislamu kwa kusherehekea sikukuu hiyo ambayo ni idi ya kupata ushindi katika kutekeleza wajibu na amri ya mwenyezi Mungu na kueleza kuwa, anatarajia viongozi wa nchi za Waislamu wataweza kukabiliana na sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja, ubeberu wa tawala za kiistikbari na ugaidi kote duniani kwa kuwa na umoja na mshikamano zaidi na hivyo kutayarisha njia ya kueneza zaidi amani na utulivu katika kanda hii na ulimwenguni na kuimarisha uadilifu na udugu katika Umma wa Kiislamu. 

Baadhi ya nchi za Kiislamu kama Syria, Palestina, Afghanistan, Uturuki na kadhalika zimeadhimisha sikukuu ya Idul Adh'ha leo Jumapili na nchi nyingine za Kiislamu kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinaadhimisha sikukuu ya Idi kesho Jumatatu. 

Katika sikukuu hii ya Idul Adh'ha Mahujaji wa Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu huwajibika kuchinja mnyama na kuhuisha kitendo cha Nabii Ibrahim (as) baada ya kufuzu mtihani mkubwa wa kuchinja matamanio ya nafsi yake.