Iran na Kyrgyzstan zatiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55994-iran_na_kyrgyzstan_zatiliana_saini_makubaliano_ya_ushirikiano_wa_kiusalama
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kyrgyzstan zimetiliana zaidi makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya usalama.
(last modified 2026-08-14T10:24:44+00:00 )
Sep 14, 2019 03:34 UTC
  • Iran na Kyrgyzstan zatiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kyrgyzstan zimetiliana zaidi makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya usalama.

Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Bishkek mji mkuu wa Kyrgyzstan baina ya Abdolreza Rahmani Fazli, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran na Kanali  Kashkar Janushaliev Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kyrgystan. Mawaziri hao wameeleza utayari wa nchi zao kushirikiana katika kuimarisha usalama wa eneo, kupambana na misimamo ya kuchupa mipaka na magendo ya madawa ya kulevya.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran ambaye siku ya Alkhamisi alielekea nchini Kyrgyzstan kwa shabaha ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo, amesema katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Muhakhammedkalyi Abylgaziev kwamba, amani na usalama wa eneo utapatikana kwa kuweko uhusiano mzuri baina ya mataifa ya eneo.

Abdolreza Rahmani-Fazli, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran (kushoto) akipeana mikono na Mukhammedkalyi Abylgaziev Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan

Aidha amesema kuwa, Marekani si taifa la kuaminika hata kidogo na akazitaka nchi za eneo kuimarisha ushirikiano wao na kuwa na uhusiano mzuri ili ziweze kkukabiliana na changamoto mbalimbali zinazozikabili.

Kwa upande wake Muhakhammedkalyi Abylgaziev Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan ameshukuru misaada ya Iran kwa nchi yake ambapo sambamba na kuashiria historia ya uhusiano wa nchi hizo mbili amesema kuwa, Bishkek inataka kustawishwa zaidi uhusiano na Tehran katika nyanja zote.