Iran iko tayari kutuma misaada kwa raia wa jimbo la Kashmir
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56010-iran_iko_tayari_kutuma_misaada_kwa_raia_wa_jimbo_la_kashmir
Mkuu wa Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaandikia barua mbili tofauti wakuu wa Hilali Nyekundu ya Pakistan na mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la India, akiwataarifu habari ya Iran kuwa tayari kutuma misaada ya kibinaadamu kwa wakazi walioathirika wa jimbo la Kashamir.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 14, 2019 22:07 UTC
  • Iran iko tayari kutuma misaada kwa raia wa jimbo la Kashmir

Mkuu wa Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaandikia barua mbili tofauti wakuu wa Hilali Nyekundu ya Pakistan na mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la India, akiwataarifu habari ya Iran kuwa tayari kutuma misaada ya kibinaadamu kwa wakazi walioathirika wa jimbo la Kashamir.

Katika barua hizo, Ali Asghar Peyvandi, amesema kuwa, mgogoro wa Kashmir na matukio ya hivi karibuni yaliyojiri katika eneo hilo, yameibua wasi wasi mkubwa hususan kuhusiana na hali ya raia wa kawaida. Kadhalika Peyvandi amebainisha kwamba Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa sehemu ya jamii ya kimataifa na pia kwa mujibu wa ujumbe na majukumu iliyonayo, inatangaza uwajibikaji wake katika kuwafikishia msaada wa kibinaadamu raia wa kawaida walioathirika wa eneo hilo.

Wakazi wa eneo la Kashmir ambao wanapitia wakati mgumu wa mateso na tabu

Inafaa kuashiria kuwa tarehe 5 Agosti mwaka huu, serikali ya India ilitangaza kufuta kipengee cha katiba kinachotoa fursa maalumu kwa serikali ya Kashmir iliyo chini ya usimamizi wa New Delhi. Hii ni katika hali ambayo wakazi wa Kashmir wanataka kutekelezwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuitishwa kura ya maoni itakayoainisha mustakbali wa eneo hilo, lakini serikali ya India imekuwa ikipinga hatua hiyo.