Zarif: Mafuta ya Waarabu ni muhimu zaidi kwa Trump kuliko damu zao
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56130-zarif_mafuta_ya_waarabu_ni_muhimu_zaidi_kwa_trump_kuliko_damu_zao
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, siasa za Marekani kuhusiana na vita vya Yemen zimeonesha kuwa, mafuta ya Waarabu ni muhimu zaidi na yana thamani zaidi kuliko damu zao kwa serikali ya Washington.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Sep 20, 2019 03:52 UTC
  • Zarif: Mafuta ya Waarabu ni muhimu zaidi kwa Trump kuliko damu zao

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, siasa za Marekani kuhusiana na vita vya Yemen zimeonesha kuwa, mafuta ya Waarabu ni muhimu zaidi na yana thamani zaidi kuliko damu zao kwa serikali ya Washington.

Katika ujumbe wake wa Twitter uliotumwa mapema leo Ijumaa, Muhammad Javad Zarif amesema kuwa kabla ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za wapiganaji wa Yemen dhidi ya taasisi za mafuta za Saudi Arabia Washington ilikhitari siasa za kunyamazia kimya mgogoro wa Yemen kwa sababu miongoni mwa abjadi za siasa za Marekani ni: "Damu ya Waarabu mkabala wa mafuta ya Waarabu".

Amesema matokeo ya mashambulizi makali ya miaka minne ya Saudi Arabia na washirika wake huko Yemen ni kuuliwa Wayemeni zaidi ya laki moja, njaa ya zaidi ya Wayemeni milioni 20 na ugonjwa wa kipindupindu uliosawasibu raia milioni 2.3 wa Yemen.

 Amesema mkabala wake Marekani inatambua kitendo cha Wayemeni cha kulipiza kisasi kwa kushambulia taasisiza mafuta za Saudia kuwa ni hatua ya kijeshi isiyokubalika.

Muhammad Javad Zarif

Jumamosi iliyopita, kikosi cha drone cha harakati ya Ansarullah kilishambulia viwanda vya kusafisha mafuta vya Buqayq na Khurais vya shirika la mafuta la Saudia, ARAMCO na kusababisha hasara kubwa kwa Riyadh. Mashambulizi hayo ambayo yamesimamisha nusu ya uzalisha wa mafuta yote ya Saudi Arabia, yamefanyika kujibu jinai na mauaji yanayoendelea kufanywa na watawala wa Riyadh dhidi ya raia wa Yemen.