Jeshi la Iran liko tayari kukabiliana na vitisho vyovyote vya adui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56520-jeshi_la_iran_liko_tayari_kukabiliana_na_vitisho_vyovyote_vya_adui
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Jeshi la Iran liko tayari kukabiliana na kila aina ya vitisho ambavyo adui amevipanga"
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 10, 2019 00:49 UTC
  • Jeshi la Iran liko tayari kukabiliana na vitisho vyovyote vya adui

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Jeshi la Iran liko tayari kukabiliana na kila aina ya vitisho ambavyo adui amevipanga"

Meja Jenerali Sayyid Abdulrahim Mousavi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran aliyasema hayo jana Jumatano katika mazoezi ya kijeshi ambayo hayakuwa yanatarajiwa ya jeshi la nchi kavu katika eneo la Maghairbi mwa Iran. Ameongeza kuwa: "vikosi hivi vilipokea amri ya oparesheni usiku (wa kuamkia Jumatano) na punde baada ya hapo mazoezi yakaanza na yanaendelea vizuri."

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran amezungumzia kuhusu ujumbe wa mazoezi hayo na kusema: "Mazoezi ya Jeshi la Nchi kavu yana ujumbe kwa taifa kubwa la Iran kuwa, jeshi lao liko tayari kabisa kukabiliana na chokochoko zozote zile tarajiwa za adui."

Meja Jenerali Sayyid Abdulrahim Mousavi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran

Meja Jenerali Mousavi ameongeza kuwa ujumbe wa mazoezi hayo kwa maadui ni kuwa, iwapo wanapanga njama, basi wafahamu kuwa, majeshi ya Iran yako tayari kabisa katika eneo au wakati wowote ule na yatasimama kidete na kwa nguvu kubwa zaidi.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa vikosi vya majeshi ya Iran viko katika kilele cha utayarifu na vitatekeleza amri yoyote kwa kasi ya juu kabisa.