Iran yapinga madai ya afisa wa Marekani kuhusu ubalozi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i57061-iran_yapinga_madai_ya_afisa_wa_marekani_kuhusu_ubalozi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepinga madai ya afisa mmoja wa Marekani ambaye amedai kuwa Iran inataka Marekani ifungue ofisi ya masuala ya visa katika Ubalozi wa Usiwishi mjini Tehran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 04, 2019 23:01 UTC
  • Iran yapinga madai ya afisa wa Marekani kuhusu ubalozi

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepinga madai ya afisa mmoja wa Marekani ambaye amedai kuwa Iran inataka Marekani ifungue ofisi ya masuala ya visa katika Ubalozi wa Usiwishi mjini Tehran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Sayyid Abbas Mousavi amekanusha kuwepo ombi kama hilo kutoka Iran.

Siku ya Jumapili, gazeti la Wall Street Journal la Marekani lilichapisha ripoti kuhusu uhusiano wa Iran na Marekani na kudai kuwa, 'afisa mmoja wa Marekani amesema hivi karibuni, Iran kupitia, Uswisi ambayo inalinda maslahi ya Washington mjini Tehran, imetaka kufuuguliwe ofisi ya kutoa huduma za visa."

 Ubalozi wa Uswisi mjini Tehran ndio unaowakilisha maslahi ya Marekani nchini Iran.

Maandamano nje ya uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran, 04 Novemba 2019 

Ikumbukwe kuwa, tarehe 4 Novemba mwaka 1979, wanafunzi wa Iran katika kulalamikia njama za Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran walivamia na kuzingira 'Pango la Ujasusi' (Ubalozi wa Marekani) mjini Tehran kwa lengo la kuzuia dola hilo la kibeberu kufikia malengo yake haramu dhidi ya mapinduzi machanga yaliyokuwa yamefikia ushindi Februari mwaka huo. Baada ya tukio hilo Iran ilitangaza kufungwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran na kutimuliwa wanadiplomasia wote wa Marekani.