Iran yashika nafasi ya pili katika mashindano ya ubunifu na uvumbuzi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i57309-iran_yashika_nafasi_ya_pili_katika_mashindano_ya_ubunifu_na_uvumbuzi_duniani
Timu ya Iran ambayo imevumbua 'glovu erevu ya kielektroniki yenye joto' imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya kimataifa ya uvumbuzi na ubunifu nchini Croatia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 16, 2019 23:04 UTC
  • Iran yashika nafasi ya pili katika mashindano ya ubunifu na uvumbuzi duniani

Timu ya Iran ambayo imevumbua 'glovu erevu ya kielektroniki yenye joto' imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya kimataifa ya uvumbuzi na ubunifu nchini Croatia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la ISNA, watafiti Wairani wamefanya uchunguzi kuhusu matatizo ya wapanda milima na watu wanaofanya kazi katika maeneo ya milimani au baridi kali, na hatimaye wamefanikiwa kuunda glovu za nano ambazo zina uwezo wa kufanya kazi kama simu ya mkononi.

Glovu hii erevu au automatiki ina uwezo wa kuchunguza alama muhimu katika uhai wa mwanadamu kama vile mapigo ya moyo, kiwango cha joto na shinikizo la damu. Aidha glovu hii ina uwezo wa kuunganishwa na mfumo wa mawasiliano wa GPS na hivyo iwapo mpanda milima atakumbwa na tatizo, ana uwezo wa kutuma ujumbe kupitia mfumo huo.

Timu ya wanasayansi Wairani waliounda glovu erevu

Glovu hii iliyoundwa na wanasayansi wa Iran inamuwezesha mtumiaji kustahamili baridi kali ya nyuzi joto chini ya 40. Wanasayansi Wairani wametumia teknolojia ya nano kuunda kitambaa kilichotumiwa kutegeneza kitambaa cha glovu hiyo.

Mashindano ya kimatiafa ya uvumbuzi na ubunifu hufanyika mjini Croatia kila mwaka katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Croatia katika mji wa Zagreb.