Iran yakosoa nchini za Ulaya kwa kuingilia mambo yake ya ndani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i57415-iran_yakosoa_nchini_za_ulaya_kwa_kuingilia_mambo_yake_ya_ndani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa hatua ya nchi za Ulaya kuingilia mambo ya ndani ya Iran na kusema: "Badala ya nchi za Ulaya kutoa matamshi ya kuingilia mambo ya ndani ya Iran na kuwaunga mkono wahuni, zinapaswa kuwajibika kuhusu kushindwa kutekeleza ahadi zao kwa watu wa Iran."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 22, 2019 03:35 UTC
  • Iran yakosoa nchini za Ulaya kwa kuingilia mambo yake ya ndani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa hatua ya nchi za Ulaya kuingilia mambo ya ndani ya Iran na kusema: "Badala ya nchi za Ulaya kutoa matamshi ya kuingilia mambo ya ndani ya Iran na kuwaunga mkono wahuni, zinapaswa kuwajibika kuhusu kushindwa kutekeleza ahadi zao kwa watu wa Iran."

Sayyid Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria matamshi ya hivi karibuni ya kuingilia mambo ya Iran ambayo yametolewa na wakuu wa Ulaya hasa msemajii wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya na kusema ni bora nchi za Ulaya awali zishughulikie matatizo ya ndani ya bara hilo. Amesema nchi za Ulaya zinapaswa kushughulikia matatizo ya watu wa Ulaya ambao kila wiki hubainisha malalamiko yao katika maeneo mbali mbali ya bara hilo.

Mousavi ameongeza kuwa: "Kile ambacho nchi za Ulaya zinapaswa kuzingatia ni kuwa zimekiuka ahadi za mapatano ya nyuklia ya JCPOA."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameendelea kusema kuwa: "Nchi za Ulaya awali zinapaswa kusema ni kwa nini zimefuata nyayo za ubabe wa Marekani katika vikwazo na ugaidi wa kiuchumi dhidi ya Iran na kisha zifafanue ni kwa nini zinatoa matamshi ya uingiliaji na machozi ya mamba sambamba na kuwatetea wahuni na walioharibu mali za umma na za watu binafsi nchini Iran."

Itakumbukwa kuwa, Ijumaa iliyopita, serikali ya Iran iliamua kukata ruzuku ya mafuta iliyokuwa ikiitoa kwa wananchi. Baadhi ya wananchi waliandamana kwa amani kulalamika kuhusu kuondolewa ruzuku hiyo lakini wahuni na vibaraka wa ajinabi walitumia vibaya malalamiko hayo ya wananchi na kuibua ghasia ambazo zimelaaniwa kote nchini.