Sisitizo la Iran la kuangamizwa kikamilifu silaha zote za atomiki
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i57509-sisitizo_la_iran_la_kuangamizwa_kikamilifu_silaha_zote_za_atomiki
Msimamo wa kimsingi na wa siku zote wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutokomezwa kikamilifu aina zote za silaha za nyuklia na kuunga mkono malengo ya Mkataba wa Kupiga Marufuku Kikamilifu Majaribio ya Silaha za Nyuklia (CTBTO).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 26, 2019 08:10 UTC
  • Sisitizo la Iran la kuangamizwa kikamilifu silaha zote za atomiki

Msimamo wa kimsingi na wa siku zote wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutokomezwa kikamilifu aina zote za silaha za nyuklia na kuunga mkono malengo ya Mkataba wa Kupiga Marufuku Kikamilifu Majaribio ya Silaha za Nyuklia (CTBTO).

Kazim Gharib Abadi, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa zenye makao yake mjini Geneva Uswisi, alisisitiza Jumatatu ya jana katika kikao cha 35 cha Kamisheni ya Utangulizi wa Mkataba wa Kupiga Marufuku Kikamilifu Majaribio ya Silaha za Nyuklia (CTBTO) juu ya msimamo wa Iran kuhusiana na suala hilo na kueleza kwamba, kufikiwa kikamilifu malengo ya mkataba na kupiga marufuku kikamilifu majaribio ya silaha za nyuklia kunafungamana na uwajibikaji wa nchi zinazomiliki silaha hizo hatari.

Mkataba wa Kupiga Marufuku Kikamilifu Majaribio ya Silaha za Nyuklia (CTBTO) ulipasishwa Septemba 10 mwaka 1969 kupitia azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Christopher Ashley Ford, Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Kimataifa na Kutoeneza Silaha za Nyuklia Katika Chuo cha Hudson anaamini kuwa: Sehemu kubwa ya changamoto za ulimwengu wa nyuklia hii leo chimbuko lake ni kuzifanya kuwa mpya silaha za atomiki na kuhuika ushindani baina ya madola makubwa katika uwanja wa nyuklia. Ni kwa kuzingatia ukweli huo, ili kufikia malengo ya mkataba huu na vile vile mkataba wa kuzuia uzalishaji na usambazaji wa silaha za nyuklia, nchi zote zilizotia saini mkataba huu zinapaswa kuheshimu na kufungamana kikamilifu na mkataba huo.

Katika kipingee cha 6 cha mkataba wa Kuzuia Uundaji na Uenezaji Silaha za Nyuklia (NPT), kumebainishwa mambo ya lazima na hatua ambazo tawala mbalimbali zinapaswa kuchuukua na kufangamana nazo katika uga wa kuachana na silaha za nyuklia. Aidha katika kipengee cha nane cha mkataba huo imebainishwa wazi kwamba, kila baada ya miaka mitano kutafanyika uchunguzi kuhusiana na utendaji wa mkataba huu kwa minajili ya kupata hakikisho kwamba, malengo ya utangulizi na vipengee vya mkataba huo vimetekelezwa.

Kwa muktadha huo, katika mikutano ya kuchunguza na kutathmini mkataba huu, mwaka 2000 kulipigwa hatua ya kimsingi iliyojumuisha hatua za kivitendo kwa shabaha ya kutekeleza kipengee cha 6 cha utokomezaji wa silaha za nyuklia, lakini licha ya kuweko maamuzi hayo, mikutano ya upitiaji upya hadi mwaka 2015 haikufanikiwa kufikia makubaliano yoyote kuhusiana na nyaraka yoyote kati ya nyaraka kuu na za asili.

Mkataba wa Kuzuia Uundaji na Uenezaji Silaha za Nyuklia (NPT), umetambua na kudhamini bila ubaguzi haki za nchi zote wanachama ikiwemo haki ya kufanya uhakiki, kuzalisha na kutumia teknolojia ya nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani. Hata hivyo kumekuwa na ubaguzi katika kutekeleza mkataba huu huku kukiwa na vizingiti vingi katika njia ya kufikia lengo hilo.

Mauaji yaliyofanywa na Marekani katika mashambuulio ya mabomu ya atomiki huko Hiroshima na Nagasaki 1945

Marekani ikiwa mmoja wa wamiliki wakubwa zaidi wa viwanda vya atomiki duniani na ikiwa muungaji mkono mkuu wa utawala haramu wa Israel wenye kumiliki mamia ya mabomu ya atomiki pasina ya kuweko usimamizi wa asasi za kimataifa kwa shughuli zake hizo za nyuklia, mwaka 1945 ilizitumia silaha hizo kwa raia wasio na hatia katika miji ya Hiroshima na Nagasaki huko Japan na kuwaua mamia ya maelfu ya watu. Athari za mashambulio hayo ya mabomu ya nyuklia zingalipo hadi leo.

Hassan John, mhadhiri wa sheri za kimataifa anasema kuwa, shambulio la atomiki la Marekani dhidi ya Hiroshima ni jinai kubwa zaidi iliyyowahi kufanywa katika historia ya mwanadamu na kuongeza kuwa, dhamira na kumbukumbu za kiutu katu haziwezi kusahau taswira haribifu, mauaji na miili iliyoungua kwa moto ya watu hususan wanawake na watoto wasio na hatia huko Hiroshima na Nagasaki.

Wataalamu wa mambo wanaamini kuwa, silaha za atomiki za Marekani ndio kizuizi kikuu cha kutekelezwa mikataba ya nyuklia. Mtandao wa wataalamu na wasomi wa atomiki umeandika katika ripoti yake kuhusiana na idadi ya mabomu ya atomiki ya Marekani kwamba: Marekani ina takribani vichwa 3800 vya nyuklia ambapo 1750 kati yake vimewekwa juu ya makombora ya balestiki huku vichwa vingine 2050 vikiweko kama akiba.

Marekani kwa kuwa na faili kama hili ilikuwa ikifuatilia kuhakikisha kuwa, jamii ya kimataifa inajiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na hivyo kuifanya ifuate mtazamo wake wa kupinga miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa malengo ya amani.

Hata hivyo, Washington imeshindwa kufikia malengo yake hayo hasa kutokana na kuwa, ripoti zote za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) zimethibitisha kwamba, hakuna ishara zozote zinazoonyesha kwamba, miradi ya nyuklia ya Iran imekengeuka mkondo wa amani.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa mmoja wa wahanga wakuu wa silaha za kemikali daima imekuwa ikisisitiza juu ya udharura wa kutokomezwa kikamilifu silaha hizi.

Gholam Hossein Dehqani, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Katika Masuala ya Sheria na Kimataifa akihutubia jana katika mkutano wa 24 wa kila mwaka wa wanachama wa mkataba wa silaha za kemikali huko The Hague Uholanzi, alitoa wito wa kuweko usimamizi zaidi wa Shirika Linalopiga Marufuku Silaha za Kemikali kwa mwenedo wa utokomezaji silaha za kemikali za Marekani na utawala ghasibu wa Israel.