Mousavi: Iran haitawasahau marafiki wake katika kipindi kigumu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58077
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haitawasahau marafiki zake wa kipindi kigumu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 24, 2019 08:20 UTC
  • Mousavi: Iran haitawasahau marafiki wake katika kipindi kigumu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haitawasahau marafiki zake wa kipindi kigumu.

Sayyid Abbas Mousavi amesema kuwa Tehran na Moscow zina uhusiano makhsusi na wa kihistoria na kuongeza kuwa: Uhusiano wa Iran na Russia umeongezeka kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni hususan baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu licha ya panda shuka zilizoshuhudiwa katika vipindi mbalimbali. 

Mousavi amesisitiza kuwa, Tehran na Moscow zina maadui lakini nchi hizi mbili jirani na zenye nguvu za Iran na Russia zitaendele kuwa pamoja.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, Iran na Russia zina ushirikiano mzuri katika duru za kimataifa na kwamba Tehran na Moscow zinafanya jitihada kubwa za kukomesha mgogoro wa Syria na kurejesha amani katika nchi hiyo suala ambalo pia litakuwa na taathira nzuri katika amani na usalama wa eneo zima la Mashariki ya kati. 

Amesema kuwa, katika mahusiano ya pande mbili pia Iran na Russia zimekuwa pamoja na zitaendelea kushirikiana licha ya vikwazo na mashinikizo ya Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla.